Itakuwa shida kubwa. Marekani wametoa dola trillioni mbili na kila Mmarekani (wakiwemo watoto wadogo) atapata angalau dola 1200 ili kujikimu angalau kwa chakula. Mabenki pia wamesitisha ishu za kurudisha mikopo angalau kwa miezi mitatu kwa watu waliokwama. Wanachotaka tu uwapigie simu na ueleze shida yako. Hata ma landlords hakuna kufukuza watu kwa sasa.
Kuna NGOs nyingi pia ambazo hupika vyakula na kuvigawa bure kwa watu homeless. Na nyingine hugawa non perishable foods kama cereal na vyakula vya kwenye makopo. Watu masikini huenda huko na kugawiwa vyakula hivi. Masupamaketi hupeleka huko pia vyakula vinavyokaribia kumaliza muda wake. Tangu quarantine ianze na watu wengi kupoteza kazi zao kuna misururu mirefu ya watu katika food banks hizi watu wakitegemea kupatiwa chakula cha bure.
Kwetu tukifikia hatua ya quarantine sijui itakuwaje masikini kwa sababu hatuna mifumo ya kueleweka na watu wengi hasa huko mijini wanategemea kwenda kuhemea kila siku ndiyo wale. Litakuwa janga kubwa sana na hata social unrest. Tuombe sana ndugu zangu hali hii isifike huko.
Quarantine siyo mbaya kama una mahitaji yote ndani. Unajidamka asubuhi unafanya vimazoezi vyako, unakula na unaendelea na mishe zingine huku ukila likes kwa raha zako. Kama huna chakula ndani hiyo ni habari nyingine aisee. Mungu Atuokoe jamani [emoji1545][emoji1545][emoji1545]