Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waziri Mkuu si mpishi wa Rais, hata tuseme kuwa maadamu Rais mwenyewe anayapenda mapishi yake, sisi wengine tusipoyapenda si kitu. Waziri Mkuu ni Mpishi Mkuu wa Tanzania nzima. Kama hatupendi mapishi yake au kuanza kutupakulia vyenye sumu, au kachoka, au kashindwa kupika, ni wajibu wetu kumwambia mwajiri wake ateue mpishi mwingine.
julius nyerere
 
Hatuwezi kuwa wakweli tukisema kuwa Rais hana hatia, Rais wa Tanzania si sawa na Malkia wa
Uingereza. Huyo ni Mkuu wa Nchi kikatiba ambaye hana madaraka ya kuongoza nchi yake. Kwa
mujibu wa Katiba na mazoea ya nchi yao hana budi akubali ushauri wa Waziri Mkuu wake, Hata kama yeye mwenyewe binafsi hakubaliani na ushauri huo. Rais wa Tanzania sivyo alivyo. Yeye ni Mkuu wa nchi Mtendaji. Kikatiba halazimiki kukubali na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu ambalo hakubaliani nalo, hasa kama tofauti yenyewe ni kwa jambo la msingi, kama vile jambo la maadili na dhamiri, au sheria, au Katiba ya Nchi
julius nyerere
 
Wakati wa mgogoro wa Zanzibar kuingia katika OIC na utaratibu wa kuchagua Makamu wa Rais,
yawezekana kuwa Rais mwenyewe aLikuwa akipendelea msimamo wa "Wazanzibari". Na hasa kuhusu suaIa la OIC, maelezo yake kwa Wazee wa Dar es Salaam na baadaye alipowahutubia wananchi siku ya Mei Mosi, Mtwara, yalifanya watu wengi waamini hivyo. Na washauri wake wa karibu walitaka tuelewe hivyo: kwamba ugumu wa suala la OIC ulikuwa unaletwa na Rais mwenyewe, maana alikuwa akiliona suala hila kwa jicho la Uzanzibari, badala ya kuliona kama Rais wa Tanzania na mlinzi mkuu wa katiba yake.
julius nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…