Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Luis Suarez huyu ni staa wa soka wa timu ya taifa ya Uruguay ambaye kwa sasa anaichezea FC Barcelona ya Hispania, akiwa na umri wa miaka 12 Suarez alikuwa akicheza mpira pekupeku kutokana na familia yake kushindwa kumudu kumnunulia viatu, Suarez amezaliwa katika familia ya watoto saba yeye akiwa wanne na akiwa na umri wa miaka 9 baba na mama yake walitengana, Suarez wakiwa Montevideo aliendeleza kipaji chake kwa kucheza mtaani lakini pia alikuwa akifanya kazi za kufagia mtaani.
 
Luka Modric huyu ni moja kati ya viungo bora wa timu ya taifa ya Croatia na club ya Real Madrid ya Hispania lakini akiwa na miaka 6 mwaka 1991 vita vya Croatia ambavyo vilimpelekea baba yake kuungana na jeshi vilimfanya yeye na familia yake kwenda kuishi Kolovare katika kambi ya wakimbizi kwa miaka saba.
 
Carlos Tevez amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama West Ham na Man United na sasa yupo kwao Argentina anaichezea Bocca Junior, Tevez amekulia Fuerte Apache nchini Argentina moja kati ya sehemu hatari zaidi na wanaishi watu masikini na kuna matukio mengi ya kiharifu na uuzwaji wa dawa za kulevya, kuharibika kwa meno yake kunatokana na matukio ya ugomvi aliyokuwa anapitia katika mtaa aliokulia.
 
Cristian Ronaldo ni moja kati ya wanamichezo matajiri katika hii dunia kwa sasa na mara yake ya kwanza anapanda ndege ilikuwa ni wakati anakwenda kusaini Man United, kabla ya hapo Ronaldo amekulia katika familia ya kimasikini Ureno na ilifika wakati akawa analala chumba kimoja na dada zake kutokana na ugumu wa maisha licha ya kuwa umri ulikuwa unataka awe na chumba chake.
 
Dani Alves amecheza FC Barcelona, Juventus na sasa PSG ya Ufaransa, Alves wakati akiwa mdogo alikuwa akilazimika kuamka saa 10 alfajiri ili kwenda na baba yake kumsaidia katika shughuli zake za kila siku na alikuwa akilala katika kitanda kibaya, pamoja na ugumu wa maisha hayo aliyoyapitia Alves amewahi kukiri kuwa alikuwa ameridhika nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…