Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bundesliga itaanza kuchezwa kukiwa na mashabiki uwanjani kuanzia msimu mpya wa 2020/21, kwasasa wachezaji wa vilabu 36 Ujerumani vya Ligi Kuu na daraja la kwanza wameanza mazoezi na Bundesliga ndio itakuwa Ligi ya kwanza kuanza kuchezwa.
 
Rafael Nadal

- Real Madrid

Supastaa wa mchezo wa tenisi, Rafael Nadal hajawahi kabisa kuficha kuhusu mapenzi yake na klabu ya Real Madrid. Mhispaniola huyo amekuwa akiishabikia Los Blancos kwa muda wote wa maisha yake na amekuwa akiifuata timu hiyo kwenye mechi zake. Jambo hilo limemfanya hata apigiwe debe la kuwa rais wa klabu hiyo wakati Florentino Perez atakapong’atuka. Nadal amekuwa akiishabikia pia timu ya mtaani kwao, Mallorca. Alikuwa moja wa watu wenye hisa kwenye klabu hiyo mwaka 2010 alipojaribu kuwasaidia kipesa, lakini timu ya mapenzi yake ya dhati ni Los Blancos. Nadal humwaambii kitu kuhusu Real Madrid.
 
Back
Top Bottom