Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wala hawana wasiwasi. Kila kitu kinaenda poa ni kama hakuna kabisa ishu ya corona pale Old Trafford. Kitu wanachokimisi ni mechi za ligi tu. Tangu Ed Woodward, atue Old Trafford mwaka 2005, uchumi wa United, umekuwa tu ukiimarika kila mwaka.
 
Kukosekana kwa mechi, wala sio tatizo kama ilivyo kwa Barcelona inayotegemea mapato ya mlangoni. United, yenye wafanya kazi 900, sio kama imepuuza wazo la kupunguza wafanyakazi huko baadaye, lakini janga hili halioneshi kuwasukuma kufanya hivyo hivi karibuni
 
Kuna taarifa klabu za EPL, zinasubiri tamko kutoka kwa mabosi wa Shirikisho la soka Uingereza (FA) na umoja wa wachezaji (PFA), ambao walikutana Ijumaa, lakini kwa United, wala hawana presha kwani hawategemei mapato ya mlangoni na matangazo ya runinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…