Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maynor Figueroa (Houston Dynamo)

Gwiji wa Honduras, Figueroa, ambaye alikuwa akifunga mabao matata kabisa kwenye Ligi Kuu England akiwa na Wigan, amekuwa akitamba kwenye Ligi Kuu Marekani kwa miaka ya karibuni. Amekuwa gumzo huko. Kwa sasa anatamba kwenye kikosi cha Houston Dynamo baada ya kuhama kutoka Colorado Rapids na FC Dallas, ambako alikuwa moto wa kuotea mbali. Mashabiki wa England, wamemsahau Figueroa, lakini huko Marekani anawapa raha tu kwa sasa.
 
Emre Belozoglu (Fenerbahce)

Kiungo mchezeshaji, Emre, 39, bado anacheza soka lake kwenye Ligi Kuu Uturuki, ambapo mwaka jana alirudi kuichezea Fenerbahce kwa mara ya tatu kwenye maisha yake ya soka. Kitu ambacho utashangaa ni kwamba bado amekuwa akipata nafasi kwenye timu ya taifa ya Uturuki, akicheza zaidi ya mechi 100 katika kikosi hicho. Kwenye ubora wake, Emre alikuwa bonge la staa katika soka la Ulaya, lakini alikuwa kimya kwa miaka ya karibuni kuwafanya mashabiki wake kumsahau, lakini Emre bado anakipiga Fenerbahce.
 
Milan Baros (Banik Ostrava)

Fowadi huyo wa zamani wa Liverpool, Milan Baros, ambaye alishinda Kiatu cha Dhahabu cha michuano ya Euro 2004, amerudi kwao Jamhuri ya Czech na sasa anaitumikia timu ya Baník Ostrava. Akiwa na umri wa miaka 38, Baros bado amekuwa mtumishi bora kabisa ndani ya uwanja, ambapo kwenye kikosi hicho cha Ostrava, amefunga mabao 15 katika mechi 44 alizochezea timu hiyo tangu aliposajiliwa 2017. Baros ni moja ya washambuliaji matata kabisa waliowahi kutokea kwenye chama la Anfield.
 
Salomon Kalou (Hertha Berlin)

Fowadi wa Ivory Coast mwenye medali ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Salomon Kalou alijiunga na Hertha Berlin ya Ujerumani mwaka 2014 na yupo kwenye kikosi hicho akicheza zaidi ya mechi 150. Kalou alikuwa bonge la staa alipokuwa kwenye kikosi cha Chelsea, kabla ya kwenda kukipiga Hertha, mahali ambako amefunga zaidi ya mabao 50 katika misimu yake saba kwenye kikosi hicho. Kalou hadi sasa bado yupo kwenye kikosi cha Hertha Berlin huku mashabiki wake wengine wakiwa wamemsahau mchezaji huyo kutokana na ukimya wake.
 
Maxi Rodriguez (Newell’s Old Boys)

Winga huyo wa Kiargentina alifunga mabao 15 katika mechi 57 alizoichezea Liverpool na sasa yupo kwao anachezea timu yake ya utotoni ya Newell’s Old Boys kwa mara ya tatu katika maisha yake ya soka. Amekuwa na msimu mzuri pia, akifunga mabao tisa msimu huu kabla ya kutundika daruga zake. Lakini, jambo kubwa ni kuwafanya mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia alipokuwa na jezi za wababe wa Anfield, kwamba mchezaji huyo bado anakipiga hadi sasa.
 
Keisuke Honda (Botafogo)

Kiungo huyo wa Kijapani, Keisuke Honda yupo kwenye kikosi cha Botafogo ya Brazil, huku akiwa kocha wa timu ya taifa ya Cambodia. Honda alikuwa na kipindi kizuri alipokuwa kwenye kikosi cha AC Milan, ambapo alilifanya jina lake kuwa kubwa kwenye soka la Ulaya. Baada ya kuwa kimya na wengi wakiamini kwamba huenda Mjapaji huyo amestaafu soka, lakini ukweli ni kwamba bado anakipiga huko Brazil katika kikosi cha Botafogo. Honda ni moja ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa kwenye soka la Italia.
 
Claudio Pizarro (Werder Bremen)

Utashangaa, lakini huo ndio ukweli kwamba straika huyo wa Peru, bado anacheza kwenye kikosi cha Werder Bremen – akiwa na umri wa miaka 41. Ni jambo nadra sana kuona washambuliaji kuendelea kucheza wakiwa na umri huo, lakini kwa mkali huyo wa zamani wa Chelsea na Bayern, ambaye alitangaza kwamba atastaafu soka mwishoni mwa msimu huu bado anaendelea kukipiga kwa sasa. Ligi ya Bundesliga imesimama kutokana na janga la corona, lakini ukitazama mechi za Breman utaona huduma ya Pizarro.
 
Fabio Quagliarella (Sampdoria)

Fowadi huyo veterani bado anacheza soka la kiwango cha juu akiwa na umri wa miaka 37, akiwa amefunga mabao tisa na kuasisti mara mbili akiwa na kikosi cha Sampdoria msimu huu. Straika huyo Mtaliano siku zote amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kwenye Ligi Kuu England hasa katika nyakati alizokuwa kwenye ubora wake, lakini uhamisho huo hautatokea tena kutokana na umri kumtupa mkono na watu kama wamemsahau kama bado yupo anakipiga.
 
Michael Essien (Sabail)

Staa mkubwa kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England. Kiungo wa zamani wa Ghana, Michael Essien alikuwa moto wakati alipokuwa akikipiga Chelsea na alikwenda kucheza soka la kiwango cha juu Real Madrid. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka zaidi ya 37 aliwahi kuzitumikia pia Panathinaikos na Persib Banding ya Indonesia kabla ya sasa kuitumikia klabu ya Sabail ya Azerbaijani iliyoanzishwa miaka minne tu iliyopita. Kwa hiyo, Essien bado anacheza.
 
20200417_091230.jpg
,
 
Back
Top Bottom