Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sifa ya Kuzuia Kansa

Jaribio lililofanyika juu ya panya na watafiti Taasisi ya Utafiti wa Kansa, Tata Memorial Center, Mumbai, India kumenukuliwa uwezekano wa athari ya binzari kuzuia kansa ya tumbo na ngozi. Jaribio kubwa la utafiti wa athari za binzari kwenye kuzuia kansa ulifanyika kwenye kansa ya utumbo mkubwa (colon cancer) ambapo aina nyingine za kansa kuhusiana na curcumin kwa sasa bado zipo njiani.
 
Inazuia Ugonjwa wa Alzheimer's

Ugonjwa wa Alzheimer's (Alzheimer's disease au Senile dementia) ni ugonjwa unaoendelea ambao unaharibu kumbukumbu na kazi nyingine za akili. Vinavyounganisha seli za ubongo na seli zenyewe zinadumaa na kufa, hatimaye kuharibu kumbukumbu na kazi nyingine muhimu za akili.
 
Tafiti iliyofanywa na Srikant Mishra kutoka 'Departmentbof Neurology, Plummer Street, Sepulveda, CA, curcumin ina uwezo mkubwa wa kusafisha au kuondoa protini iitwayo amyloid kwenye mishipa ya damu, ambayo kiashiria kikuu cha muendelezo wa ugonjwa wa Alzheimer. [7] Jaribio lingine lililofanyika pia limegundua kwamba virutubisho mbadala vyenye binzari huimarisha hali mwili na uwezo wa utambuzi kwa watu wenye umri mkubwa wasio na matatizo kumbukumbu.
 
Faida Nyingine

Faida nyingine za binzari na curcumin ni kama zifuatazo:

Huzuia homa ya Uti wa Mgongo na hupunguza maumivu

Virutubisho mbadala vyenye binzari (Turmeric supplements) mara nyingi hushauriwa vitumike kwa kupunguza maumivu uti wa mgongo, gout, na maumivu ya misuli yaliyotokana na mazoezi au ajali. Utumiaji wa mara kwa mara wa binzari unaweza kutibu tatizo. Curcumin pia husaidia kwenye kupunguza matatizo yanayopelekea kuzeeka kama atherosclerosis, kulingana na tafiti iliyochapwa kwenye jarida la 'Immunity and Ageing
 
Hutibu Msongo wa Mawazo

Curcumin kiukweli ni kitu muhimu sana, na tafiti zimeweza hata kujaribu athari zake kwenye kudhibiti homoni ndani mwili.Tafiti zimeonyesha kwamba curcumin ina athari sawa na Prozac kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali ya mwili kulegalega, wasiwasi, na stress. Hii inaifanya kuwa mbadala wenye nguvu kwa madawa ya hospitali, ambayo mara nyingi yana hatari ya au athari mbaya baada ya kutumia.
 
Watu wenye magonjwa ya moyo huwa wanashauriwa kuitumia sana na kama wasipoweza kuipata basi watumie supplements. Kachupa kadogo ka vidonge vyake au maji huuzwa kwa dola 37 madukani.
Huko kijijini kwa bibi imeoteshwa karibu na mkokoa,hadi mwezi wa sita ndio inachimbuliwa kwa ajili ya kuupendezesha wali na samaki mbelele...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…