Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Face Mask: Binzari imekuwa ikitumika kwenye kufanya face mask toka zama za zamani kutokana na kuboresha ngozi na kuzuia harara. Inaweza kuchanganywa na maziwa mtindi, asali, aloe vera, au vitamin E.
 
Skin Moisturizer: ngacc Binzari iliyochanganywa na mafuta mzeituni (olive oil) au mafuta ya nazi (coconut oil) hutengeneza ngozi ya asili yenye kuvitia, ngozi hubakia na unyevu bila kukauka mara kwa mara.
 
Matumizi ya Mapishi

Binzari pia ni kiungo maarufu kwenye supu, sauces, curries, msosi wa nyama, maandalizi wa mchele, na hutumika kama kiungo chenye kuleta ladha kwenye chakula kwa zaidi ya dazani ya vyakula vingine vya kitamaduni.
 
Maziwa: Maziwa ya moto yaliyochanganywa na binzari (kijiko cha chai) inasaidia kupata nafuu kutokana na homa, baridi, na hufanya kazi kama sedative (-enye kukufanya usinzie, u-relax, utulie) ya asili.
 
Madhara

Ijapokuwa si kitu kilichozoeleka kusababisha allergy, binzari inaweza kuleta madhara kwenye mwili, hasa ukiitumia kwenye kiwango kikubwa. Madhara hayo ni kama yafuatayo:

Kichefuchefu
Kizunguzungu
Kuhara
 
Kwenye baadhi ya kesi, matumizi yaliyopitiliza ya curcumin kwenye kiwango cha dawa yamesababisha mapigo ya moyo kupiga tofauti. Pia, inaweza kuzolotesha kuganda kwa damu kwa kuongeza athari za dawa zinazozuia damu kuganda. Kwa maana hiyo, watu wenye shida ya kuganda kwa damu au wenye kutumia dawa za kufanya damu kuwa nyepesi ni lazima kuepuka binzari. Mara zote ongea na wataalamu kabla ya kuongeza kitu hiki chenye nguvu kwenye diet yako, na kumbuka --kila kitu kinatakiwa kichukuliwe kwa wastani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…