Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.zipo pilipili za kuwasha kama pilipili mbuzi na pilipili kichaa lakini pia zipo ambazo haziwashi kama pilipili hoho, hivyo kama wewe ni muoga wa pilipili za kuwasha basi kula hata pilipili hoho ili ufaidike na faida nyingi sana zinazopatikana kwenye vyakula hivyo.zifuatazo na faida muhimu zinazopatikana kwenye pilipili.
 
kiasi kikubwa cha vitamin c; utafiti umeonyesha kwamba pilipili zina kiasi kikubwa cha vitamin c kuliko hata kile kinachopatikana kwenye matunda kama machungwa na machenza, vitamin c ni nzuri kwa kinga ya mwili, na kulainisha ngozi.
 
husaidia kupunguza uzito; pilipili huongeza kasi ya mwili kufanya kazi na kuchoma mafuta[metabolism], kemikali ya piperin iliyoko kwenye pilipili huzuia mwili kutengeneza mafuta mapya, lakini pia zenyewe zikiwa na ujazo mdogo wa ndani kiasi kwamba hata ule nyingi kiasi gani haziwezi kukuongeza uzito, kumbuka pilipili unazowezakula nyingi ni zile ambazo haziwashi.
 
hukinga mishipa ya fahamu; pilipili za aina mbalimbali hua na vitamin b6 ambayo ni muhimu sana katika afya ya mishipa ya fahamu, ukosefu wa vitamin hii ni moja ya vyanzo vikuu vya kupata ngazi mwilini na kuhisi dalili za kuwaka moto.
 
hutunza macho; lutein ni enzyme inayopatikana kwenye pilipili, katika umri mkubwa wa maisha hufanya kazi ya kuzuia kutokea kwa mtoto wa jicho[cataract],huu ni weupe unaotokea kwenye lens ya jicho na kumfanya mtu apate upofu.
 
husaidia mmeng'enyo wa chakula; pilipili husaida mwili kutengeneza kiasi kikubwa cha kemikali ya hydrochloric acid inayopatikana tumboni ambayo kazi yake ni kuongeza mmeng'enyo wa chakula hivyo kuupa mwili virutubisho vyote muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…