KAI HAVERTZ
Kiungo mchezeshaji wa Bayer Leverkusen, Kai Havertz amezivutia timu nyingi za Ligi Kuu England kuanzia Manchester United, Liverpool na sasa Chelsea. Kocha wa Chelsea, Frank Lampard baada ya kunasa saini ya kiungo wa Ajax, Hakim Ziyech amekuwa bize kusaka saini ya wachezaji wa safu ya ushambuliaji na hapo anampigia hesabu Havertz. Lakini, mchezaji huyo yupo kwenye mipango ya Liverpool na Man United, ambao wanahaha pia kunasa saini yake. Klabu nyingine ya nje ya Ligi Kuu England inayohitaji saini ya Havertz ni Bayern Munich na ni kama kawaida yao ya kuhakikisha wanasajili wachezaji wote wanaotamba na timu nyingine kwenye Bundesliga.