Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hee arsenal daah pole mkuu,hawa watu wanakimbilia chipukizi zaidi. Tetesi za hivi karibuni hizi hapa
We Numbi inaonekana uko vizuri kwenye michezo haswa ligi ya ulaya, ebu niambie timu yangu ya asernal vipi hakuna tetesi zozote za uhakika wa kununua mchezaji mpya wa mana, nipe ripoti

Sent using Jamii Forums mobile app

Arsenal inataka kumsaka kiungo wakati wa Bayern Munich Angelo Stiller, 19. (Bild - in German)

Arsenal huenda ikalazimika kuuza wachezaji wake sita ili kupata pesa za kulipa pesa zilizosalia kwa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe euro milioni 72 kwa hatua yake ya kutoka Lille msimu uliopita. (Sun)

Washika bunduki wanapendelea kumsajili mchezaji wa RB Leipzig, Dayot Upamecano, 21, kiwapiku Tottenham na Manchester United, ambao pia wanamtomlea macho mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ulinzi .(Football.London)

Matumaini yaArsenal ya kumsajili beki wa kushoto Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain yamezimika , mchezaji huyo atamwaga wino kukipiga katika klabu ya Barcelona. (Le 10 Sport -in French)

Wakala wa Henrikh Mkhitaryan amekana taarifa kuwa Arsenal inampango wa kumuuza mchezaji huyo raia wa Armenia. Mino Raiola amesema tetesi kuhusu kiungo huyo wa kati, 31, ''si za kweli'' (Express)

Washika bunduki hao pia wako njiani kuingia makubaliano na mchezaji huru George Lewis. Winga huyo wa Norway mwenye miaka 19, alikuwa akiichezea Tromso. (Metro via Goal)

Arsenal wanaweza kupewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 27, ikiwa ni mbadala wa mshambuliaji Pierre- Emerick Aubameyang, 30. Mkataba wa Aubameyang unatarajiwa kumalizika msimu ujao, wakati Icardi anacheza kwa mkopo Paris St-Germain. (Tuttosport via Teamtalk)

Real Madrid wameambia Arsenal kufanya uamuzi kufikia tarehe 15 mwezi Juni iwapo wako tayari kumuuza mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake (Sunday Mirror)
 
Basi tu Numbi timu tunaipenda sana ila, hawajui na sisi tumemis kakikombe pale Emirates jaman,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…