Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] akili za usiku hizo. Ila hiyo tabia kwenye picha nilikuwa naichukia balaa, hivi bado watu wanafanya? Halafu hufanywa na wababa wale watu wazima wanaopenda vitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado ipo,kabla corona haijaingia vizuri limbaba naliheshimu balaa kulipa mkono wa salamu likafanya hivyo nilikerekaaaa
 
*CHAPATI ZA MTINDI* Mahitaji:- Unga wa ngano 1/2 kg Samli 1/4 kikombe Chumvi kjk 1 1/4 cha chai Juice ya chungwa 1 Ganda la chungwa 1 lilokunwa Sukari kjk 1 chai Maziwa ya unga 1/4 kikombe Mtindi kikombe 1 Ute wa mayai 2 *JINSI YA KUPIKA* 1.Tia mahitaji yote isipokuwa samli katika bakuli kisha kanda kufanya unga mlaini na wa kuvutika. 2. Tia samli kisha kanda tena kwa dk 5-10. Funika acha ukae kwa muda wa nusu saa 3. Sokota chapati zako kama kawaida kisha acha madonge yakae kwa muda wa nusu saa. 4. Choma chapati zako, hakikisha moto ni medium heat ili upate rangi nzuri.
 
TAMARIND AND GINGER JUICE / JUISI YA UKWAJU NA TANGAWIZI : Mahitaji : Ukwaju kiasi Sukari robo Hiliki ya unga kijiko 1cha chai Maji kiasi Tangawizi mbichi 1/2 kijiko cha chai iliosagwa Maelezo : Chemsha ukwaju, ukipoa ,weka tangawizi na ufikiche pamoja na ukwaju kisha ukamue rojo lote. Kisha uchuje. Chukua rojo la ukwaju uliochujwa ongezea maji kiasi na weka na hiliki tia pamoja na sukari kisha koroga mpaka sukari ikolee vizuri. Weka katika fridge ikipata baridi tayari kwa kunywa na vitafunio au chakula chochote upendacho.
 
CURRY POWDER MAHITAJI

1.Pilipili nyekundu kavu - 20 hadi 30

2.Giligilani - 1/2 kikombe

3.Mdalasini-vijiti 4 vikubwa

4.Hiliki- punje 15

5.Karafuu kijiko 1 cha chakula

6.Pilipili manga nzima - kijiko 1 cha chakula

7.Manjano-kijiko 1 na nusu cha chakula

8.Bizari nyembamba vijiko 3 vya chakula

9.Shimari vijiko 3 vya chakula

MATAYARISHO

1.Tia mahitaji yote kwenye sufuria kasoro manjano.

2.kaanga moto mdogo kwa dakika 10 hadi 12.

3.Acha ipoe.

4.Tia kwenye blenda ya kusagia vitu vikavu pamoja na manjano saga hadi iwe unga.

5.Hifadhi vizuri kwenye kopo na tumia wakati wa kupikia mchuzi.

6.Inakaa muda mrefu tu.Masala za kutengeneza nyumbani ndio nzuri zaidi.
 
JINSI YA KUPIKA PILAU LQ KUKU SIMPLE NYUMBANI. MAHITAJI NA VIPIMO i. Mchele wa basmati - 3 vikombe ii. Kuku - ½ iii. Viazi - 4 iv. Vitunguu - 2 v. Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu vi. Binzari ya pilau nzima - 1 Kijiko cha chakula vii. Binzari ya pilau - ½ kijiko cha chai viii. Pilipili manga nzima - ½ kijiko cha chai ix. Karafuu nzima - 8 x. Iliki nzima - 6 xi. Mdalasini nzima - 5 vijiti xii. Pilipili mbichi iliyosagwa - 2 xiii. Chumvi - kiasi xiv. Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 1. Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele. 2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi. 3. Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria. 4. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. 5. Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo 6. Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia. 7. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza) 8. Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.
 
JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI SANA. MAHITAJI NA VIPIMO. i. Unga mweupe wa ngano vikombe 4 ii. Samli safi vijiko 3 vya kulia iii. Chumvii kijiko 1 chai iv. Maji vuguvugu (warm) vikombe 2 v. Samli ya kupikia chapati. NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 1. Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja. 2. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga. 3. Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano hivi. 4. Finika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi hivi kwa kuufunika ili hewa isiingie. 5. Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo. 6. Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati. 7. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba. 8. Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote. 9. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo. 10. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo. 11. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote. 12. Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi 13. Pika chapati kwenye frying pan moto wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha kulia cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri. 14. Endelea namna hii huku unafuta frying pan na kitambaa kisafi au karatasi za jikoni (tissue) baada ya kila chapatti. KIDOKEZO. 1. Unapomaliza kuzipika kila moja, zitandaze kwanza chapati katika sahani (au sinia) kubwa zipate kupoa ziwe kavu ili zisinyonyanye mafuta. Kisha tena ziweke katika sahani yako ya kawaida. 2. Ni nzuri kutolea na jam au asali 3. Unaweza ku freeze chapati katika Freezer bags. Kunja chapati moja moja ziwe nusu. Zifunike na Wax paper, kisha zitie kwenye freezer bags na uzihifadhi katika freezer. Unapotaka kula, toa kwenye freezer na upashe moto
 
MAMBO 10 YA KUZINGATIA KATIKA USAFI WA JIKO LAKO.

1. Hakikisha unasafisha jiko lako mara kwa mara kabla na kila baada ya kumaliza kupika. Usafi uwe wakina,futa sehemu zote kutoa vumbi na wakati wa kupiga deki piga kwa umakini kwa kusogeza v na kusafisha kila kona usifanye juu juu.
 
. 2. Jokofu pia ni sehemu ambayo ina ushawishi mkubwa sana wa bacteria ikiwa haina matunzo, hivy hakikisha unapitia mara kwa mara kuhakiki ni safi na imepangwa katika mpangilio sahihi. Panga bidhaa zako kwa mpangilio usirundike ili kuhakikisha usalama na kutunza uhalisia wa kila bidhaa,penda zaidi kuhifadhi mabaki ya vyakula katika kontena za mifuniko kabla ya kuhifadhi ktk jokofu ili kuepusha Muingiliano wa harufu wa vyakula.
 
3. Panga jiko lako kwa mpangilio sahihi, hakikisha kila chombo kinakaa sehemu husika usiache vitu vinazagaa zagaa chini au ju ya jiko au counters bila mpangilio. Unapomaliza kupika basi jiwekee desturi ya kuondoa kila kitu na kurudisha pahala pake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…