Hawana namna nyingine ila isipokuwa wanaomba muda urudi nyuma wasahihishe makosa.Makosa yaliyozaliwa na chaguzi za kukata tamaa.Walipokutana na punje moja ya mchanga waliogopa kusonga mbele.Wakizani ni lazima mbele ya safari kuna jangwa kubwa likiwasubiri.Lah hasha.Kuishi hakuko hivyo.Kuishi ni sayansi,kuishi ni majaribio, kabla ya hitimisho fanya upembuzi wa kutosha.Mimi na wewe tungali tuna muda,tungali tuna afya,tungali tuna akili,tungali tuna pumzi.Tukiunganisha vyote hivi hakika safari yetu haitavunjika na zaidi sana tutakutana ana kwa ana na bahari iliyosheheni lulu.Lulu Isiyo ndogo kwa vipimo,wala ndogo kwa kimo.Hii itakuwa sawa sawa na mapenzi yetu.Italingana na ndoto zetu,itafanana na juhudi zetu.Lulu hii haitakuwa na upendeleo.Itatii kiu kadri ya kila mmoja alivyothubutu ,kadri ya kila mmoja alivyoitafta.