Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jihadhari kuwaamini wana siasa kupita kiasi.
Wanasiasa walinivuruga siku niliposhuhudia mtu aliyeitwa fisadi kwa miaka 8 akipewa fursa ya kugombea urais kwa njia ya mkato bila kumshindanisha na yeyote.
Tangu hapo nimedharau sana siasa.
Sijawahi kumuamini mwanasiasa achilia mbali hiyo 'kupita kiasi'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jihadhari kuwaamini wana siasa kupita kiasi.
Wanasiasa walinivuruga siku niliposhuhudia mtu aliyeitwa fisadi kwa miaka 8 akipewa fursa ya kugombea urais kwa njia ya mkato bila kumshindanisha na yeyote.
Tangu hapo nimedharau sana siasa.
Kosa kubwa sana pengine kuliko yote katika siasa (za upinzani) Bongo. Hata heka heka zinazoendelea huko ukichunguza vizuri chanzo chake kikuu kimojawapo ni hiki. Chama kilichokuwa makini kufumba na kufumbua kikapoteza nguzo mojawapo ya sera zake kuu (kupambana na mafisadi) na kubakia kuwa chama cha kudandia matukio tu bila kuwa na sera mama endelevu na falsafa jumuishi. Leo hii hata matunda kiliyovuna katika vuguvugu lile yanapukutika moja baada ya jingine (wenyewe wanasema yananunuliwa [emoji16]). Ni muda wa kurudi, kama wanavyosemega wenyewe, kwenye drawing board....
 
Jihadhari kuwaamini wana siasa kupita kiasi.
Wanasiasa walinivuruga siku niliposhuhudia mtu aliyeitwa fisadi kwa miaka 8 akipewa fursa ya kugombea urais kwa njia ya mkato bila kumshindanisha na yeyote.
Tangu hapo nimedharau sana siasa.
Nadhani waliovurugwa vizuri na huyu mtu ni wale walipiga deki barabara ili mzee wa kichwa cheupe apite[emoji3526]
Walipiga deki weee utadhani punda mwanapunda mfalme anapita .

Kuna jamaa yangu mmoja kutwa kucha kwenye maandamano ya mzee..basi alivyo mfupi [emoji3526]..akawa anainukia kucha amuone mzee.

Matokeo yake mzee akarudi zake CCM
Sijui waliwaambia nini watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye umenipa sababu ya kwanini Russia iljipenyeza kimyakimya kumfanyia kampeni hatimaye kumsaidia apate ushindi kwenye uchaguzi uliopita huyu bwana Trump.
Hata sasa wanampambania sana ashinde kwa mara nyingine na mimi naamini kuwa atashinda hiyo Novemba. Huyu mgombea wa Democrat ni mzee mno halafu ni kama vile hayuko sawa kichwani. Miaka mingine minne ijayo basi Trump atakuwa amefanikiwa kuirudisha Amerika "nyumbani" na japo bado pengine itaendelea kuwa na masilaha makali na jeshi lenye nguvu kuliko mataifa mengine lakini kama vita vya Iraq na Afghanistan vilivyotuonyesha, maguvu ya kijeshi pekee siyo kigezo pekee cha kuwa mbabe wa dunia. Ushawishi wa kidiplomasia pia ni muhimu sana. Yaani ukisema jambo tu unasikilizwa. Unaheshimiwa. Na heshima hii unaipata kwa kuwa kwenye mikataba mingi pamoja na kuonyesha uwezo wako wa kiuchumi. Ndiyo maana Amerika ilikuwa ndiye mchangiaji mkuu katika mashirika mengi ya kimataifa na mtoa misaada mkuu duniani kote. Trump hataki yote haya na sera yake kuu ni Amerika kuangalia kwanza maslahi yake ya ndani. Lakini hata huku ndani kwenyewe ukiangalia vizuri sana sana kimsingi ni maslahi ya wazungu tu.

China na Urusi wakichanga karata zao vizuri huu ndiyo wakati mzuri wa kuibuka na kujitandaza duniani kote kama wanavyofanya katika nchi za Kiafrika. Na huu ndiyo unaweza kuwa mwanzo wa mmojawao kuwa supa pawa. Walichokuwa wanakipigania wakati wa vita baridi sasa wanaweza kukipata bure bila kurusha kombora la Nyuklia hata moja!
 
Wewe hukupiga deki au ulikuwa bado mdogo?

By the way, shikamoo [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…