Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuweza kuona nafasi za ziada za kuboresha maisha -"opportunities", kwani kiasili hatutengenezi "opportunities" bali tayari opportunities zipo, ila tunachofanya ni kuzitambua, na kuanza kuzitumia.
 
Haijalishi ubunifu ni wa namna gani - iwe kuandika kitabu, kuzalisha vyakula, kutoa huduma za ufundi n.k , yote hayo yanaweza kufanyika kwa ubunifu na kuleta manufaa.
 
Haijalishi ubunifu ni wa namna gani - iwe kuandika kitabu, kuzalisha vyakula, kutoa huduma za ufundi n.k , yote hayo yanaweza kufanyika kwa ubunifu na kuleta manufaa.
 
Zingatia hatua zifuatazo:-

1. Jifunze kulikubali tatizo kama changamoto na fursa ya kuleta suluhisho: Wapo wengi ambao wanapoona ugumu katika jambo fulani, wanasita kuendelea au wanasubiri suluhisho toka kwa wengine.
 
Ni kweli kuna mambo utawaachia wengine, lakini lile 'lililo karibu' na uwezo wako waweza litatua. Mfano ukaribu ninaozungumzia hapa inawezekana ni mazingira unayoishi, aina ya ujuzi wako, na uwezo wako
 
2. Tumia muda wa kutosha kujifunza: Ili kuwa mbunifu inakupasa uwe na taarifa za kutosha kuhusu tatizo unalotaka kutatua, ujue pia wengine wamefanya nini.
 
Ndio maana STEVE JOBS aliwahi kusema :-
“Creativity is just connecting things. When you ask creative people how they did something, they feel a little guilty because they didn’t really do it, they just saw something. It seemed obvious to them after a while. That’s because they were able to connect experiences they’ve had and synthesize new things. And the reason they were able to do that was that they’ve had more experiences or they have thought more about their experiences than other people".
 
Twaweza kutafsiri hivi:
"Ubunifu ni namna tuu ya kuunganisha vitu. Ukiwauliza watu wabunifu waliwezaje kufikia walivyofanya, wanajisikia hatia kwakuwa kiukweli hawakufanya lolote, bali waliona tuu kitu fulani. Ilionekana wazi kwao baada ya muda fulani. Hiyo ni kwa sababu waliweza kuunganisha uzoefu waliokuwa nao, na kuweka vitu kwa pamoja.Na sababu ya wao kuweza kufanya hivyo ni kuwa walikuwa na uzoefu, au walitumia muda mwingi zaidi kufikiria kuliko watu wengine, kuhusu uzoefu wao".
 
3. Thubutu Kuota: Baada ya kulitambua tatizo, ukawa tayari kulitatu, ukajawa na hamasa ya kujifunza, na ukajifunza vya kutosha kuhusu hali husika, kinachofuata ni wewe sasa kufikiria suluhu ya tatizo husika.
 
Back
Top Bottom