myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Aiseee...Mara kadha mwaka 1972, ‘Dourado [mwanasheria Mkuu Wolfgang Dourado aliyekuwa mwendesha mashtaka ] akija katika chumba cha kuhojiwa’, Khamis aliniambia, ‘husoma maelezo yaliyoandikwa na baadae kusema, “Inabidi mumkamue zaidi mtu huyu”, yaani mateso zaidi. Mahakamani alisema, “mikono yao ilisokotwa tu, basi,” kusema kweli, maelezo ya Dourado juu ya mada hii yanastahili kunukuliwa yote kwa ukamilifu. Yanaonyesha mtazamo wa matukio yanayofanana na hayo ya hivi sasa katika kesi za wale walioshtakiwa kwa mujibu wa sheria za ugaidi za Uingereza na Marekani. Hapa pia, matumizi ya ushahidi uliopatikana kwa njia ya mateso ni jambo la kawaida.
View attachment 1460050
Aisee....Ni wazi kuwa nia ya serikali ya Zanzibar ilikuwa ni kuwaweka watu hawa gerezani maisha. Kama Hamed alivyonambia:
Kuhoji kuliendelea lakini wapelelezi weledi kutoka bara hawakuweza kupata lolote la kumtia mtu hatiani. Kabla ya mauaji washtakiwa walikwenda kuvua samaki. Hapajakuwepo na silaha ndani ya mashua yao – isipokuwa chakula tu! Kila kitu kilionyesha kuwa hawakuwa na hatia lakini hilo halikuwa na umuhimu kwasababu wale waliokuwa madarakani walichodhamiria ilikuwa ni kuendesha kesi ya maonyesho ili kuwasingizia ubaya washtakiwa na kuonyesha kuwa kuanzia sasa na kuendelea, wapinzani wote watasagwasagwa kikatili.
======
hassan nassor moyo
View attachment 1460055
Duh!!Karume Akabidhi Vibaraka Wake Madaraka ya Jeshi
Akielewa kuwa angelilihitaji jeshi ili kulinda nafasi yake, Karume aliliunda upya jeshi hilo ili kukabidhi madaraka kwa vibaraka wake aliowaamini sana. Katika kipindi cha mara tu baada ya mapinduzi, wanachama wa Chama cha Umma Party ambao walikuwa Cuba walifanyakazi kwa juhudi kubwa ili kulianzisha jeshi la Zanzibar, Jeshi la Ukombozi la Zanzibar.
Lakini mamlaka ya kidikteta ya Karume yalipozidi kukua alianza kuwaona watu hawa kuwa ni tishio. Kama Shaaban alivyonambia, ‘Karume alitaka tuwe pembeni. Kwa hivyo mwezi Julai 1964 kati yetu sisi 18 ambao tulipata mafunzo Cuba tulipelekwa Urusi kwa kipindi cha mwaka mmoja’ (mahojiano na Shaaban, 2009).
Sawasawa...Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua na maumivu ya tumbo.