Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1586718121361.jpeg
 
Kwa maisha yetu hususani mijini ni vigumu kulima mbogamboga nyumbani hivyo tumekua tukitegemea mboga za kununua ambazo mara nyingine zimekua si salama kwa matumizi ya binadamu kutokana na maeneo zinapolimwa hata maji yanayotumika kumwagilia.
 
Hivyo ifike pahala wewe mwenyeweze uweze kulima mbogamboga nyumbani kwako. Acha visingizo kwani inawezekana kuwa mkulima wa mbogamboga mwenyewe nyumbani kwako kwa kutumia ndoo ambazo hazitumiki tena, mabeseni hata vyungu ambavyo hutumika kupanda maua. Vifaa ambavyo nimevieleza hapo juu ndivyo ambavyo vitakusaidia wewe kuweza kulima mbogamboga nyumbani kwako.
 
Jinsi ya kupanda:
Chukua makopo yako au vyungu kulingana na idadi unayotaka kupanda
Panda mbegu ya biringanya moja au mbili kwa kila kopo.Mwagilia vizuri na weka mbolea kila baada ya wiki mbili. Unaweza kuvuna baada ya 16 mpaka 24 baada ya kupanda baada ya kuona ngozi ya nje inang’aa na haina mikunjo.
 
Jinsi ya kupanda:
chagua kopo ambalo ni refu kwenda chini, Tafuta udongo wenye rutuba ambao hauna mawe, inafaa zaidi udongo wa kununua kwa sababu udongo wa kuchukua popote huwa hauna rutuba ya kutosha na huwa unavimelea vya kuua mmea.
 
Ukipanda jitahidi kumwagilia mara kwa mara usiache udongo ukauke kabisa mwagilia angalau mara moja kwa wiki maana maji mengi yataozesha mizizi
Weka mbolea kuanzia wiki ya 5-6 baada ya kupanda.Karoti zitakua tayari kuvunwa baada ya miezi miwili na nusu au vile utakavyopendelea ziwe kulingana na matumizi yako.
 
NYANYA

Jinsi ya kupanda• Kwa kutumia makopo yako weka udongo kwa kila kopo.
• Baada ya kuweka udongo changanya na mbolea vizuri
• Kwa kila kopo moja panda mche moja wa nyanya au mbegu
• Mwagilia vizuri baada ya kupanda miche yako kwa mfululizo siku za kwanza na endelea kumwagilia miche mpaka itakapokua
 
Back
Top Bottom