Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anaitwa George Junius Stinney, Jr. alizaliwa Oktoba 21, 1929 na kufariki kwa kunyongwa Juni 16, 1944 akiwa na umri wa miaka 14 tuu. Ni mtoto, muamerika mweusi maarufu sana duniani kutokana na simulizi yake ya kusikitisha ya hukumu ya uonevu juu ya kosa lisilo lake. Anajulikana zaidi kwa tukio la kupewa hukumu isiyo yake, hukumu ya kifo ya kuonewa ya kuhusika na vifo vya mabinti wawili weupe wa umri wa miaka 7 na 11 mwaka 1944 huko Alcolu, South Carolina alikokua akiishi na familia yake. March 23, 1944 watoto wa kizungu Betty Binnicker (11) na Mary Thames (7) walipatikana wamefariki karibu na kiwanda cha mafuta mjini Alcolu, South Carolina, baada ya kutorudi nyumbani mapema. Polisi wakamkamata George aliyekuwa akiishi karibu na kumlazimisha akiri kosa, maelezo yote 'feki' ya kukiri kosa yaliandikwa katika notebook, ndani ya dakika 10 tuu za kusomwa kesi hiyo mahakamani George alihukumiwa kifo huku akinyimwa kujieleza chochote. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa March 24 siku moja tuu baada ya watoto hao kukutwa wamefariki ni kwamba walibondwa vichwani na chuma kizito ambacho kwa vyovyote kwa umri wa George asingeweza kabisa kukinyanyua chuma hicho, lakini kikafichwa. Toka anakamatwa hadi ananyongwa ilikuwa ni ndani ya miezi mitatu kasoro, kwa muda huo wote wazazi wake waliruhusiwa kumuona George mara moja tuu, na hawakuwahi mruhusu ajitetee kwa lolote. Historia imemtaja George kuwa ndiye muamerika wa kwanza mwenye umri mdogo kuwahi kuhukumiwa kifo na kunyongwa katika historia ya taifa hilo kubwa duniani, mwaka 2014 mahakama ilikiri kuwa mtoto huyo alinyongwa kwa kuonewa. Mapitio ya kesi yake yalianza tangu mwaka 2004 ambapo kwa miaka 10 yote uchunguzi ulikuwa ukifanywa na hatimae mwaka 2014 ikabainika kuwa mtoto George hakua na kosa, alipewa hukumu ya kifo kwa kuonewa ikiwa ni miaka 70 imepita.
 
400012200203_265527.jpg
 
Back
Top Bottom