LISEMWALO lipo wanasema. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anasemekana amepanga kuwapiga bei mastaa wake kibao dirisha la majira ya kiangazi litakapofunguliwa ili kupata pesa za kusajili wachezaji wapya kuanza kukifuma upya kikosi hicho.
Hivyo Saliba na Luiz watakuwa nguzo mpya kwenye safu ya mabeki, wakati kocha Arteta atakapopitisha fagio kuondoa wale anaodhani wanapaswa kuondoka ili kutengeneza kikosi kipya kitakachokuwa na vijana wengi.
Kiungo Lucas Torreira ni staa mwingine atakayefunguliwa mpango wa kutokea baada ya mchezaji huyo mwenyewe hivi karibuni kukiri anataka kwenda kuichezea Boca Juniors. Torreira amecheza mechi 33 msimu huu na kufunga mabao mawili.
Granit Xhaka ni mchezaji mwingine anayehusishwa na mpango wa kuondoka huku Arsenal ikidaiwa kuwa kwenye hatari ya kumpoteza pia Matteo Guendouzi. Kiungo huyo kinda amecheza mechi tatu tu kwa dakika 90 chini ya Arteta.
Arsenal pia wamepanga kupunguza bili ya Pauni 350,000 kwa wiki wanayomlipa Ozil ili kupunguza gharama, huku miaka hiyo ya Emirates ikipanga kumsajili staa wa Feyenoord, Orkun Kokcu kuja kuchukua mikoba yake.
Aubameyang mkataba wake umebakiza mwaka mmoja na atauzwa mwisho wa msimu huu kwa mkwanja unaoanzia Pauni 20 milioni kwenda juu, huku staa Lacazette akiwa kwenye rada za Inter Milan.
Arsenal pia watakuwa na kazi ya kutafuta kipa wa kuja kumsaidia Bernd Leno - baada ya kuwapo kwa ripoti Emiliano Martinez atafunguliwa mlango wa kutokea. Kama hilo linalosemwa likifanyika, basi Arsenal itakuwa imeuza kikosi kizima.
PESA ndo kila kitu? La hasha, si kila kitu. Hebu cheki, Liverpool wamebakiza mechi mbili tu za ushindi kati ya tisa zilizobaki wanyakue ubingwa wa Ligi Kuu England kwa msimu huu.
Takwimu mpya zinaonyesha Manchester City ndiyo timu iliyotumia pesa nyingi zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita, ikiwa ni mara sita ya kiwango ambacho Liverpool imetumia kwenye usajili ndani ya muda huo.
Liverpool hivi karibuni walijiondoa kwenye mbio za kumnasa straika Timo Werner kwa sababu hawakuwa tayari kulipa Pauni 54 milioni kuvunja mkataba wake huko RB Leipzig.
Huo ni mfano, kikosi hicho kinachonolewa na Jurgen Klopp hakika kawaida ya kutumia pesa nyingi kuliko inazoingiza kipindi chote cha miaka mitano iliyopita.