Bendi hizo kama si zote zinazotamba nchini humo kwa sasa, ziliasisiwa na wanamuziki ama waliotoka ndani ya bendi hii au katika bendi zilizoanzishwa na wakali waliopata kuipigia.
Zaiko Langa Langa ni bendi kongwe huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sasa, ambayo bado inaendelea kudunda licha ya wimbi kubwa la kuhamwa na wanamuziki mahiri pamoja na ushindani uliopo hivi sasa.
Kwa upande wa wanamuziki nyota wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akina Papa Wemba, Bozi Boziana, Dindo Yogo, Evoloko Ley Ley ‘Joker’, Defao Matumona, Koffi Olomide na wengine wengi, lazima utapata chimbuko lao kutoka kwenye shina la Zaiko Langa Langa.
Bendi nyingi za Isifi Lokole, Yoka Lokole, Viva la Musica, Langa Langa Stars, Zaiko Familia Dei, Choc Stars, Le Anti Choc, Le Grand Zaiko Wawa, Quartie Latin na nyinginezo nyingi, zimetoka kwenye chimbuko la Zaiko. Kwa sasa inajulikana kama Zaiko Langa Langa Nkolo Mboka, yaani ‘Wakuu wa Mji’.
Yoka Lokole iliyoanzishwa na Papa Wemba, Bozi Boziana na Mavuela Somo. Grand Zaïko Wa Wa iliyoanzishwa na Felix ‘Pepe’ Manuaku Waku aliyeungana na Shimita El Diego na Djo Poster.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.