Alizaliwa mwaka 1880 katika kijiji cha Fumba huko visiwani Zanzibar.Mara alipozaliwa alipewa jina la 'Mtumwa'. Hii ni kwa kuwa alizaliwa katika kipindi cha Utumwa wa Kiarabu waliomuwa wakatwala visiwa hivyo.
Jina la Siti alipewa na Kabaila mmoja wa Kiarabu wakati huo.Baba yake bwana Saad alikuwa ni wa kabila la Kinyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga.
Wazazi wote hao walizaliwa Zanzibari. Yaelezwa kwamba hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana.Walijishughulisha zaidi katika kilimo na ufinyanzi, kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.
Kama waswahili wasemavyo “kuzaliwa masikini si kufa masikini” Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hicho kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza.
Kama waswahili wasemavyo “kuzaliwa masikini si kufa masikini” Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hicho kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza.
Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo.
Mnamo mwaka 1911, aliona ni bora ahamie mjini Unguja, ili kubooresha maisha yake zaidi. Ujio wake wa mjini humo ulikuwa wa neema kwani alikutana na bwana mmoja wa kundi la muziki wa Taarabu la ‘Nadi Ikhwani Safaa’ aliyeitwa Muhsin Ali.
Katika kipindi hicho kundi hilo ndilo lilikuwa pekee la muziki wa taarabu, lililoanzishwa na Sultani aliyekuwa akipenda starehe na anasa, bwana Seyyid Barghash Said.
Nadi Ikhwani Safaa’ lilikuwa ni la wanaume peke yake, wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni.
Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa ‘Nadi Ikhwani Safaa’ ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonesho mbalimbali katika jamii.
Kama nilivyosema moto wa Siti ulikuwa si wa kuusogelea karibu, mwaka 1928 Kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice yenye makazi yake huko Mumbai nchini India, ilisikia umaarufu wa Siti binti Saadi.