Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyimbo nyingi ziliimbwa lakini huu ndio uliovuma sana:
Siti binti Saadi kawa mtu lini,
Kaja mjini na kaniki chini,
Kama si sauti angekula nini?
Na yeye kwa kujua hila za wabaya wake, akaona isiwe taabu akajibu shambulio kwa namna hii:
Si hoja uzuri,
Na sura jamali,
Kuwa mtukufu,
Na jadi kebeli,
Hasara ya mtu,
Kukosa akili.
 
Mwanamke huyo alipofika alikutana na tajiri mmoja ambaye alijifanya amempenda. Hivyo akamchukua na kulala naye halafu baadaye akamuua.
Tajiri yule alishitakiwa kwa bahati nzuri walikuwepo mashahidi wawili walioshuhudia tukio lile. Lakini kwa vile ni tajiri huyo alitoa hongo, kesi ikawageukia wale mashahidi na wakafungwa.
 
Siti akatoa wimbo huu :
Tazameni tazameni,
Eti alofanya Kijiti,
Kumchukua mgeni,
Kumcheza foliti,
Kenda naye maguguni,
Kamrejesha maiti.
Siti aliendelea kumwambia katika nyimbo zake kwamba asijethubutu kwenda Dar er Salaam kwa maana watu wenye hasira wanamsubiri na wameapa kwa ajili yake.
 
Back
Top Bottom