KESHA LA ASUBUHI
Alhamisi 18/06/2020
*MAWAZO YA UPENDO NYUMBANI*
*Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.* 1Yohana 4:12
📝 Fanya mazingira ya nyumbani kwako yanukie kwa mawazo ya wema. Nyumbani yapasa pawe
kituo ambapo kuna upendo safi kabisa. Amani, utulivu, upendo na furaha vinapaswa kuhifadhiwa kwa ustahimilivu kila siku, hadi vitu hivi vya thamani vikae mioyoni mwa wanafamilia.
📝 Sababu ya kuwepo wanaume na wanawake wengi wenye mioyo migumu duniani ni kwa vile upendo wa kweli umechukuliwa kuwa ni udhaifu na umekuwa ukipondwa na kukandamizwa. Sehemu kubwa ya aina ya watu wa daraja hili imepotoshwa na kulemazwa wakati wa utoto, na kama mwali wa nuru ya mbinguni hautalainisha ubaridi wao na ubinafsi wa ugumu wa moyo, furaha ya mtu huyo imezikwa milele. Ili tuwe na mioyo ya upole, kama ambao Yesu alikuwa nao alipokuwa duniani, na huruma njema, kama ya malaika kwa wanadamu wenye dhambi, tunapaswa kujenga wema wa utotoni ambao ndio usahili.
📝 Wapongeze watoto wako wakati wowote unapoweza. Fanya maisha yao yawe ya furaha kadri iwezekanavyo. Changamsha moyo wako kwa kuonyesha upendo na huba, hivyo unauandaa kwa ajili ya mbegu ya ukweli...Mungu huipatia ardhi si tu mawingu na mvua bali nuru nzuri ya jua, ikisababisha mbegu iote na maua yachanue.
📝 Jicho la heri, neno la kutia moyo au kupongeza, vitakuwa kama nuru ya jua mioyoni mwao, mara nyingi hufanya siku nzima kuwa ya furaha.
🔘 *Furaha ya mume na watoto inapaswa kuwa ya kuheshimiwa zaidi kwa kile mke na mama kuliko ya wengine wote.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️