myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Muda wa pipii....
Kesi hii ni ya kwanza inayohusu mtu kurudishwa katika Afrika, kufunguliwa katika Tume ya Afrika, lakini hii si kesi ya aina ya pekee kwani ushahidi unaendelea kujitokeza kuhusiana na tabia ya kimataifa ya kurudisha watu. Kesi hii ni sehemu ya madai yanayozidi kukua ya kutambua na kutoa haki kwa watu walioathiriwa kwa kurudishwa ambayo hayataondoka. Nchi – kama Djibouti – zinazoshirikiana na Marekani katika mipango yake ya kurudisha watu, huku zikikiuka sheria zao wenyewe pamoja na Mkataba wa Afrika kwa mchakato huo, inabidi lazima ziwajibishwe na Tume ya Afrika. (Interights, 2011)
Kikwete, Rais wa Tanzania ameweka wazi kuwa si kama anataka ushirikiano wa hivi sasa juu ya kupambana na ugaidi uendelee tu bali anataka ushirikiano huo upanuliwe zaidi. Ameainisha hasa katika maeneo ya mafunzo na msaada wa kitaalam kutoka katika Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani, Wizara ya Fedha, Wizara ya Sheria na mashirika mengine na kusema kuwa anataka kuzipanua program kama hizo. Kabla ya ziara ya Rais Kikwete ya 17-18 Mei, tuliitaka Washington kuandaa mapendekezo yenye kulingana na maslahi ya Rais Kikwete. (Ubalozi wa Marekani, 2006c)
[Wakati mkakati wa kipaumbele wa kwanza wa Marekani nchini Tanzania ni] kujenga uwezo wa Serikali ya Tanzania wa kupambana na ugaidi na kuendeleza usalama … Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya juhudi za dhati katika kuanzisha kituo chake cha kupambana na ugaidi. Tarehe 4 Disemba mpango wa msaada wa kupambana na ugaidi wa [ Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani] ulizindua warsha ya wiki tatu Dar es Salaam ili kufanya majadiliano ya kina na viongozi wa Tanzania juu ya namna ya kuanzisha na kukipatia vifaa kitengo kama hicho. Ulikuwepo ushiriki wa kikamilifu wa serikali ya Tanzania wakiwemo washiriki kutoka polisi, jeshi, uhamiaji, usalama wa taifa, forodha na benki. Kwa mujibu wa wakufunzi wa Mpango wa Msaada wa Kupambana na Ugaidi walioendesha warsha kama hiyo huko Senegal, Kenya na Chad, maafisa wa Tanzania wameonyesha kwamba ‘wameshaumiliki’ mpango huo kikamilifu na kuwa wapo tayari na wana nia ya kuingia katika juhudi za utekelezaji wake. (Ubalozi wa Marekani, 2009a)