Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

acha tuendelee na simulizi ilioandikwa na comrade fulani kupitia kitabu chake (wakomunisti wa zanzibar kipindi hicho)
=======================================
Uingiliaji Kati wa Marekani Zanzibar na Bara Hivi Sasa

Tokea mwaka 2003, wakati Benjamin Mkapa alipokuwa Rais, serikali ya Tanzania ilikuwa tayari inahusika sana katika vita dhidi ya ugaidi na kwa amri ya Marekani ikifanya vitendo vya utekaji nyara na ‘urudishaji watu usio wa kawaida’. Tukio moja ambalo limejitokeza na ambalo hivi sasa lipo kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Raia ni lile la Al-Asad, raia wa Yemen aliyekuwa akiishi na kufanyakazi Tanzania tokea mwaka 1985.
 
Alikamatwa nyumbani kwake Dar es Salaam mwezi Desemba 2003, na kusokomezwa ndani ya ndege iliyokuwa ikimsubiri na kupelekwa nchini Djibouti ambako hakuwahi kufika hapo kabla katika maisha yake yote. Huko aliwekwa kizuizini ndani ya gereza la siri na kwa mujibu wa Interights kituo cha kimataifa kinacholinda haki za kisheria za binadamu, alihojiwa na kachero wa Wamarekani na kuteswa. Baadaye alipelekwa kiwanja cha ndege ambako alikutana na ‘kikundi cha warudishaji’ – kundi la watu waliovalia mavazi meusi ambao walimvua nguo na kumshambulia, kabla ya kumfunga minyonyoro na kumfunika kitambaa usoni na kumlazimisha kuingia ndani ya ndege nyengine.
 
Aliwekwa kizuizini katika magereza ya siri ya Shirika la Ujasusi la Marekani nchini Afghanistan na Ulaya ya Mashariki na hatimaye kupelekwa Yemen mwaka 2005. Aliachiwa mwaka 2006, bila ya kufunguliwa mashtaka ya kosa lolote linalohusiana na ugaidi. Kwa mujibu wa Solomon Sacco, wakili wa Interights anayeishughulikia kesi hiyo:

 
Kesi nyengine ambayo pia inaonyesha kuhusika kwa Tanzania katika kurudisha watu kusiko kwa kawaida ni ile ya Laid Saidi, raia wa Algeria. Ni moja ya kesi nyingi zinazoelezewa katika ripoti ya Shirika la Jamii Iliyo Wazi (Open Society Foundation) (2013). Saidi, raia wa Algeria, alikamatwa mwezi Mei 2003 na polisi wa Tanzania, na baada ya kukaa siku tatu gerezani Dar es Salaam alisafirishwa kwa gari hadi kwenye mpaka na Malawi na kukabidhiwa kwa maafisa wa Malawi waliokuwa wamevaa sare.
 
Alikabiliwa na mateso ya kisaikolojia na kudhalilishwa kabla ya kusafirishwa na kupelekwa Afghanistan katika hali ya kutisha. Akiwa Afghanistan alizuiliwa katika magereza matatu ya Shirika la Kijasusi la Marekani pamoja na lile ovu maarufu ‘Gereza la Kiza’ na lile la ‘Shimo la Chumvi’. Kiasi cha mwaka mmoja baadae, alisafirishwa kwa ndege hadi Tunisia ambako aliwekwa kizuizini kwa siku 75 nyengine kabla ya kurudishwa Algeria ambako aliachiwa huru.
 
Tokea Kikwete aingie madarakani mwezi Desemba 2005, Tanzania imekuwa ni mshiriki mwenye hamasa kubwa zaidi katika ‘vita dhidi ya ugaidi’. Alifafanua msimamo wake katika mkutano wake na balozi wa Marekani Retzer mwezi Mei 2006:

 
Wakati ambao Kikwete yupo madarakani, mchango wa Afrika Mashariki katika mtandao wa kimataifa wa ’vita vya Marekani dhidi ya ugaidi’ kama inavyobainisha kesi ya Al-Asad, umezidi kushika kasi na miundombinu ya kusimamia kazi ya kupambana na ugaidi ambayo kwa kiwango kikubwa inagharamiwa na nchi za Afrika ya Mashariki zenyewe imeshamirishwa zaidi. Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi cha Yemen kinachukuliwa na Marekani kuwa ndiyo mfano bora katika kazi hii.
 
Kwa mfano, balozi wa Marekani Mark Green mwezi Februari 2008 aliandika katika ‘maelezo mapya kuhusu suala la ugaidi Tanzania.

Kuanzishwa kwa Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi Tanzania ni suala la kipaumbele kwa Tanzania … Hata hivyo, mipango na muda wa kiutekelezaji wa kituo hicho vinaendelea taratibu sana kwasababu ya ukosefu wa fedha. Ili kuongeza uelewa wa Serikali ya Tanzania juu ya faida za Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi, mwezi Oktoba 2007 Ofisi ya Mratibu wa Vita dhidi ya Ugaidi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, 2001-09) iligharamia safari ya afisa mmoja wa [Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania] kitengo cha kupambana na ugaidi na afisa mmoja wa Kitengo cha Kupambana na Ugaidi cha Jeshi la Polisi la Taifa ili kukitembelea Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi cha Yemen mjini Sanaa. Kutokana na ziara hii, maafisa wote wawili wametambua juu ya ulazima wa kukikamilisha Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi cha Tanzania, na kuajiri watumishi wake kikamilifu. Hata hivyo, uhaba wa fedha bado umebakia kuwa ni kizingiti. (Ubalozi wa Marekani, 2008c)
 
Ilipofika mwezi Juni 2009, Marekani ilifurahishwa zaidi na kupiga kifua kwa Tanzania juu ya ‘vita dhidi ya ugaidi’. Kama alivyoripoti Balozi Retzer katika ‘matayarisho ya ziara ya Naibu Waziri Lew nchini Tanzania’:

 
Udhalilishaji wa Waislamu katika Afrika ya Mashariki unazidi na unahalalishwa kwa kizingizio cha kupambana na ugaidi, huku maafisa wa Marekani wakidai kuwa watu wanaohusika wanahusiana na uripuaji kwa mabomu wa balozi za Marekani mjini Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1982.[2] Wakati huo huo kumekuwa na habari za marejeo kadha kuhusiana na mahusiano baina ya watu wa ‘mwambao wa Waswahili’ na mahusiano baina ya watu wa Zanzibar, kupitia Mombasa hadi Somalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…