Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mujibu wa Lenhardt, sifa zote zinafaa zimwendee Kikwete, kwasababu:

 
Ujenzi wa ‘Vyanzo’ na ‘Nyenzo’
Katika kipindi cha vita baridi, shughuli nyingi za siri za Marekani zilikuwa ni za matumizi ya ‘vitendo vya mauaji ya moja kwa moja’. Vitendo kama hivi vimeimarishwa zaidi ili vitumike katika vita dhidi ya ugaidi, hasa wakati wa utawala wa Obama. Kama lilivyoandika gazeti la The Nation mwezi Juni 2010, vikosi maalum vinavyofanyakazi kwa ajili ya Kikosi cha Pamoja cha Shughuli Maalum vimewekwa wakati wa utawala wa Obama nchini ‘Iran, Jojia, Ukraine, Bolivia, Paraguay, Ecuador, Peru, Yemen, Pakistani na Filipino … nchi za mstari wa mbele kwa vikosi hivi, hivi sasa, kama vyanzo husika vinavyoeleza, ni Yemen na Somalia’ (Scahill, 2010).
 
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post (kama lilivyonukuliwa na Scahill):

 
Shughuli hizi za kijeshi, kama zile za wakati wa vita baridi, zinahitaji mitandao ya makachero na namna nyengine kama hizo za ujasusi katika eneo husika. Charles R. Stith, balozi wa Marekani nchini Tanzania kutoka mwaka 1998 hadi 2001, alitilia mkazo umuhimu wa mitandao na vyanzo kama hivyo.

 
Kinachohusishwa na shughuli kama hizo za kijasusi ni ufuatiliaji wa Waislamu wenye kuonyesha ishara za upinzani kwa Marekani. Hii ni shughuli iliyozidi kupamba moto baada ya 9/11, kama alivyoandika Mahmood Mamdani:

 
Marekani na Uingereza wamezidi kuanzisha programu walizozigharamia pesa nyingi ili kujaribu kuwatengeneza ‘Waislamu wazuri’ kama hao ambao wataziunga mkono nchi za magharibi. Mpango wa Mazungumzo ya Wananchi ni mmoja wa miradi kama hiyo. Kama alivyoeleza Karen Hughes, Naibu Waziri wa Shughuli za Serikali mwaka 2006 mpango huo ulikuwa:

 
Kama simu za WikiLeaks zinavyoonyesha, hata hivyo, namna hiyo ya kuwafikia watu haikuwa ikikubaliwa mara zote. Katika tukio moja, Wamarekani Waislamu ambao walikuwa ni sehemu ya program ya Mazungumzo ya Wananchi waliokuwa katika matembezi ‘kwa mshangao walizuiwa wasiingie msikitini jijini Dar es Salaam.’ Walipojaribu kuingia msikitini kundi la watu lilikusanyika na kuwazuia wasiingie huku wakiwapinga kwasababu walikuwa Wamarekani. Baadaye, wageni hao waliambiwa ‘na viongozi wa waislamu wenye siasa za wastani wa Dar es Salaam kwamba ‘vijana wenye siasa kali’ labda Waislamu wenye siasa kali wanaosaidiwa na Iran, ndio waliohusika na tukio hilo (Ubalozi wa Marekani, 2007c).
 
Juu ya yote haya, wanadiplomasia wa Kimarekani wanadhani kuwa huko visiwani wamefanikiwa katika eneo hili. Mwezi Juni 2009 katika ‘maandalizi ya ziara ya Jacob Lew’ ulisisitizwa umuhimu wa kupata ‘Baraka’ za wananchi: ‘Kazi yetu Pemba – kisiwa chenye Waislamu wengi na mfano mzuri wa mkakati huu’, ilielezwa. ‘Tumeunganisha shughuli za miradi ya kudumisha utamaduni, kukarabati misikiti ya kihistoria, miradi ya kujitolea ili kuboresha maisha ya watu vijijini na mradi mkubwa wa Shirika la Misaada la Marekani wa kudhibiti malaria na programu za elimu.’ (Ubalozi wa Marekani 2009 a)
 
Vijana Imara’ na Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Huko Zanzibar, kama ilivyo mwahali mwengine, kuzidi kwa ubaguzi dhidi ya Waislamu duniani kote, na mashambulizi ya nchi za Magharibi katika nchi zenye Waisilamu wengi, na ukatili wanaofanyiwa Waislamu katika nchi hizi na nchi nyengine kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, yamechangia katika kuwafanya Waislamu wajitambue. Zaidi ya hayo, hapa pia kuna mbinu zinazotumika kila wakati kuonyesha, hasa kwa ajili ya watalii, kuwa biashara ya utumwa asili yake inahusiana na Uislamu na Waarabu.
 
Kwa mfano, Michael Retzer, mwanasiasa wa Chama cha Republican na balozi wa Marekani nchini Tanzania aliingiwa na wasiwasi kuhusiana na habari zifuatazo ambazo alizituma kwa simu ya upepo Washington tarehe 24 April, 2006:

 
Retzer aliendelea kueleza kuwa alifanya uchunguzi zaidi kwa kufanya mikutano ya siri na ‘watazamaji wa kuaminika wa siasa za Zanzibar’ ili kuelewa zaidi juu ya masuala haya. Dk. Rwekaza Mukandala, mkurugenzi wa Asasi Isiyokuwa ya Kiserikali ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) alikuwa ni mmoja wa watu hao. Retzer aliripoti juu ya maoni yake kuwa ‘vijana wa CUF wanakosa uvumilivu na wanatafuta uongozi ‘ ingawa Hamad alikuwa bado akipendwa, hasa Pemba. ‘Kuna Wapemba ambao ni watiifu mno kwa Hamad kiasi kwamba wanadai kuiona sura yake kwenye mwezi!’
 
Juu ya kuhakikishiwa na Dk. Mukandala kuwa uwezekano wa vijana hao wasioridhika kujitenga na Chama cha CUF ni mdogo, Retzer bado alikuwa na wasiwasi kama alivyoandika katika ripoti yake kuwa ‘kutokuchukuliwa hatua huku na kukosekana kwa mkakati wa kisiasa, pamoja na kuripuka kwa hasira za vijana kunahitaji kuangaliwa kwa makini’.

REDET ilimweleza balozi kuwa jibu la matatizo hayo ni kuwepo kwa ‘elimu ya vijana na mafunzo ya uongozi ikiwa ni mkakati wa muda mrefu wa kuandaa viongozi wa baadae’. Mukandala alimwambia kuwa hili ni jambo ambalo Marekani inaweza kusaidia, kwa kukipatia kizazi kijacho cha viongozi wa Zanzibar nyenzo za ujuzi wa kushauriana na wa kushughulikia migogoro.
 
Ni wazi kuwa REDET ilifurahi kushirikishwa katika kutoa kizazi kijacho cha viongozi wa Zanzibar wanaoipendelea Marekani. Retzer aliripoti kuwa alikuwa na nia ya kuandaa programu ya ziara ya kundi la wageni wa kimataifa mwaka unaofuata kwa viongozi vijana wa CUF na CCM.
 
Kama ilivyofichua WikiLeaks, Marekani ina hamu ya kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Tanzania itakayoijumuisha CUF. Hii si kama itawanyanyua viongozi wa sasa tu, kuondoa uwezekano wa kuwa na vijana wenye siasa kali na kuleta ‘utulivu’, bali serikali kama hiyo vile vile itakuwa na fursa ya kuiwezesha Marekani kushirikiana na viongozi na wafuasi wa CUF.

Kwa mujibu wa mtoaji habari mwengine, Dk. Ndumbaro kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na rafiki mkubwa wa Dk. Mukandala kwenye REDET, ni rahisi kufanyakazi pamoja na wanachama wa CUF ‘kwani CCM bado inalazimika kutengeneza mazingira mazuri ili sekta binafsi istawi … wafanyabiashara wengi na wachuuzi ni wafuasi wakubwa wa CUF’.
 
Mambo yalikwenda taratibu katika mukhtadha huu, hata hivyo, baada ya mwaka mmoja, Retzer ambaye alikuwa akizidi kukosa uvumilivu aliendelea kuisukuma CCM kuelekea kwenye maridhiano. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe alimuhakikishia kuwa CCM, ikiongozwa na Rais Kikwete, ‘inafanyakazi usiku na mchana’ kulitatua suala hili, ijapokuwa bado vipo vikwazo viwili huko mbele: Kamati Kuu ya CCM na kukubali kwa Rais Karume kutekeleza makubaliano yoyote ya usuluhishi yatakayofikiwa’ (Ubalozi wa Marekani, 2007a)
 
Tarehe 18 Julai 2008, Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam ulifanya majumuisho ya sera yake katika waraka ulioitwa Mwongozo wa Zanzibar: suala, kwa nini tunajali na lipi tulifanyalo kuhusu suala hilo’ (2008a). Katika lugha ambayo inafanana na ile ya nyaraka za siri za miaka ya 1960 zilizohusiana na ushawishi wa kikomunisti kutoka Zanzibar kuenea katika bara lote la Afrika, mwongozo huo ulieleza wasiwasi wa Marekani juu ya siasa ya Uisilamu ya Zanzibar ambayo inaweza kuenea katika sehemu nyengine za bara hili:

 
Wakati katika miaka ya 1960 ‘utulivu katika kanda’ (ambao ulikuwa na maana ya mazingira ya salama kwa mtaji wa nchi za Magharibi) ulikuwa upatikane kwa kuiingiza Zanzibar katika Tanzania, na kuimarisha nafasi ya Nyerere, katika miaka ya hivi karibuni inaonyesha ni kwa ajili ya kumuimarisha Kikwete na kuanzishwa kwa serikali ya CUF-CCM Zanzibar ili kuzima ukakamavu wa vijana wa Zanzibar ambao wameainishwa kuwa wanaoweza kuwa magaidi wa Kiisilamu.

 
Ili kuyatekeleza malengo haya na mengine, ubalozi wa Marekani ulikuwa na jukumu la kuwashajiisha Wazanzibari na serikali ya Muungano kufikia mwafaka wa kisiasa. Na waraka huo unaeleza, Marekani ilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa kuwa ‘mipango yake mipana ya misaada kutoka mashirika mbalimbali visiwani Zanzibar … inatuweka katika nafasi nzuri mbele ya watu wa Zanzibar na viongozi wa kisiasa wa kambi zote mbili, huku ikitupa fursa ya kuyazungumzia masuala ya kisiasa ya Zanzibar kama marafiki wa kweli wa watu wa visiwani’.
 
Wanadiplomasia na Wafadhili Wanajaribu Kucheza Mchezo Mchafu
Hata hivyo, njia ya kuelekea kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikuwa imejaa vikwazo na mambo ya kukatisha tamaa kwa Marekani. Ilipofika mwezi Januari 2009 Ubalozi wa Marekani ulibaini kuwa Kikwete alionekana kubadili mtazamo wake. Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara Zanzibar ‘majigambo yake juu ya uongozi wa Karume katika kuleta maendeleo ya Zanzibar yalikuwa ya kilaghai…. kwa wapinzani waliokuwa wakisikiliza na kusubiri kusikia tamko lolote juu ya mwafaka, kuwaita “walevi” hakukusaidia kitu’ (Ubalozi wa Marekani, 2009d).
 
Ili kujua maoni ya CUF, maafisa wa Marekani walizungumza na mtu waliokuwa karibu naye. Mshauri wa mambo ya nje wa CUF, Ismail Jussa ambaye alikuwa ni mshiriki wa ‘Programu ya Marekani ya Wageni wa Kimataifa’.

Jussa aliwambia watumishi wa ubalozi kuwa Kikwete hivi karibuni amebadili lafdhi yake, akitumia lugha ya kikorombwezo cha vitani cha wale wanamapinduzi waliofanya vitendo vya kikatili vya kuadhibu watu Pemba; kuwa yeye na Seif Hamad ndio ‘watu pekee wenye siasa za wastani’ waliobakia ndani ya Chama cha CUF na heshima yao, baada ya mfululizo wa majaribio yasiyofanikiwa ‘inakaribia kupotea’; na kuwa Juma Duni, Naibu Katibu Mkuu wa CUF ‘ni mtu asiyekubali usuluhishi na ndiye atakayekifanya Chama cha CUF kuchukua msimamo mkali zaidi’.

Jussa alisisitiza kuwa panahitaji iwepo tume ya kimataifa ya namna fulani itakayohakikisha kupatikana kwa ushindi wa CUF baada ya uchaguzi ulio huru na wa haki. ‘Baada ya kuchukua madaraka’, Jussa alisema, ‘CUF “itasafisha nyumba” (Ubalozi wa Marekani, 2009e).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…