Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kula vizuri; hakikisha kabla hujala chakula chochote unatafakari kama kina faida yeyote kwenye mwili wako, ulaji wa vyakula ambavyo havina faida mwilini kama pipi, biscuit, soda, na jamii zake vitakuua na kansa siku za usoni lakini pia unene ambao kimsingi huletwa na kula sana utakuletea magonjwa hatari kama kisukari na magonjwa mengine ya moyo.
 
tumia vyombo vya moto kwa uangalifu; matumizi ya vitu kama gari na pikipiki yanahitaji umakini mkubwa sana hasa ukiwepo barabarani, vijana wengi wadogo wameuawa na vyombo hivi.epuka kuendesha gari umelewa, epuka mwendo mkali, vaa helmet wakati wa kuendesha pikipiki, vunga mkanda wewe dereva au abiria na usikubali kubebwa kwenye gari au pikipiki na mtu ambaye hathamini maisha yake.usione aibu kumwambia dereva apunguze mwendo kwani umemlipa na ameshika maisha yako. na wewe usiyejua kuvitumia kajifunze kwanza chuoni ndio uanze kuvitumia.
 
shiriki mazoezi; magonjwa ambayo sio ya kuambukizwa kama kisukari, ugonjwa wa moyo, na presha husababishwa sana na maisha ya uvivu. binadamu anatakiwa afanye mazoezi angalau nusu saa kwa siku. visingizio kwamba uko bize sana ni dalili ya kukosa vipaumbele na nidhamu kwenye maisha yako.hizo hela unazotafuta usiku na mchana usipokua na afya bora utakufa uziache.
 
epuka ugomvi usio na maana; mimi nafahamu watu waliopigwa ngumi moja tu wakafa hapohapo. mwili wa binadamu ni mlaini sana. kuna sehemu ambazo zikipigwa unakufa hapohapo. jitahidi kua mtu wa kusuluhisha zaidi kuliko kukunja ngumi.watu wote waliouawa kwa kuchoma visu au kupigwa mawe walikufa kwenye mazingira haya.kama umejifunza kupigana basi pigana pale unapokua umeshambuliwa ili kujilinda sio kuanzisha ugomvi makusudi.
 
usivute sigara; sigara ni moja ya starehe ambayo haina faida yeyote kwenye mwili wa binadamu, huharibu seli za kwenye mapafu na baadae huleta kansa ya mapafu.unaeza ukasema mbona fulani kavuta mapak leo hajafa. kila mtu ana kinga yake ya mwili amabyo ni tofauti na mwingine lakini pia hakuna anayechoka kuishi...huyo unayemuona anatamba, siku akiambiwa sigara ndio iko inamuua hata kama ana miaka 90 atasikitika sana.
 
usijihusishe na madawa ya kulevya; madawa ya kulevya hayatakuua hapohapo lakini yatakuondoa kwenye mkondo wa maisha ya mafanikio. utadharaulika na kila mtu, utakua huwezi kufanya kazi, muda mwingi utawaza kuiba ili upate madawa mengine ya kutumia.rafiki yangu mmoja mwaka 2004 alivuta bangi kwa kama miezi sita tu akawa kichaa na hajapona mpaka leo pamoja na kupelekwa hospitali nyingi za vichaa.unaweza ukaona jinsi amegeuka mzigo kwa ndugu zake.
 
jiepushe na uvunjaji wa sheria za nchi makusudi; tabia za wizi, dili za kihalifu, uuzaji wa magendo au kumuibia muajiri wako ii ufanikiwe haraka hua hazina muda mrefu sana maishani. yaani huwezi ukawa mjanja maisha yako yote kwani ipo siku utakamatwa tu.lepo hii kijana au mtu mzima ukihukumiwa miaka 30 basi maisha yako yameishia hapo na huenda ukafia gerezani. matajiri wote duniani wlianza miaka mingi iliyopita. jifunze kua mvumilivu.
 
waheshimu wazazi wako; ukisoma biblia kitabu cha kutoka 20;12 biblia inasema 'waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kua nyingi katika nchi upewayo na bwana mungu wako' sio kuwaheshimu kwa kuwapa shikamoo kila asubuhi bali kwa kufuata maelekezo na ushauri wao kwani wao wameishi miaka mingi sana duniani na wameona mengi.
 
NAMNA MSONGO WA MAWAZO UNAVOATHIRI MWILIPale mwili unavokutana na hali ya tofauti aidha kitu cha kutisha au kinacholeta mawazo ndani ya mda mfupi na tofauti hiyo ikashindwa kutambuliwa haraka na ubongo mfano pale unapokutana na samba au mnyama yeyote mkali usiyemtegemea, basi mwili hutoa kichocheo kinachoitwa cortisol ambacho kinamwagwa kwenye damu ili kuuandaa mwili aidha kupigana au kukikimbia hcho kitu.
 
Pale msongo wa mawazo unapokuwa mkubwa ndipo kinga yako ya mwili inavozidi kutohisi uwepo wa kichocheo cha cortisol ( yaani kwa lugha rahisi ni kwamba msongo wa mawazo unapunguza kwa kiasi kikubwa makali ya kinga yako ya mwili), kwa sababu kitazalishwa kwa wingi zaidi ili kuandaa mwili kupambana, na hivyo madhara yanyotokana na kutofanya kazi kiusahii kwa kinga ya mwili ndivyo yataongezeka zaidi.
 
MSONGO WA MAWAZO UNAVOSABABISHA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA KIKE NA KULETA TATIZO LA POLYCYSTIC OVARY SYNDROME.Ovary ni mfuko wa mayai ya kike, yaani mahali ambapo mayai ya kike huzalishwa.polycstic ovary syndrome au PCOS kwa kifupi ni ugonjwa unaosababishwa na kuvurugika kwa vichocheo vya kike unaowapata zaidi wanawake walioko katika kipindi cha kuzaa.
 
MSONGO WA MAWAZO KUPITILIZA UNAVOBADILI VICHOCHEO VYA KIUME VILIVYOPO NDANI YA MWANAMKE.Licha ya msongo wa mawazo kusababisha uzalishaji mkubwa wa vichocheo ndani ya mwili wa mwanamke pia vichocheo hivyo huanza kupambana na hali hiyo ya msongo wa mawazo. Hapa ieleweke kwamba msongo wa mawazo siyo kisababishi pekee cha PCOS , tatizo hilo linaweza pia kusababishwa na ulaji mbaya usiozingatia sheria za lishe bora, kutokufanya mazoezi, matumizi makubwa ya wanga na sukari na pia vyakula vilivyosindikwa na kwa ujumla mtindo mibovu na hatarishi ya kimaisha.
 
KWANINI MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHA UZITO MKUBWA NA KITAMBIKuongezeka ovyo kwa uzito,kitambi na nyama uzembe ni tatizo linalohusiana na ,msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unabadili jinsi mafuta yanavohifadhiwa ndani ya mwili kwa sababu ya kubadilika kwa vichocheona kemikali mbalimbali zinavyozalishwa na mwili pale ambapo unakuwa na stress. Kwa mfano tafiti zinasema kuwa stress kupitiliza husababisha uzalishaji wa protini inayoitwa betatrophin ambayo ni kizuizi kwa vimeng’enya ambvyo huvunjavunja mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili.
 
NAMNA YA KUPUNGUZA ATHARI ZITOKANAZO NA MSONGO WA MAWAZO
Stress ni kitu kisichoepukika kwenye maisha ya kawaida, lakini ni muhimu kufahamu na kuelewa namna ambavyo unashugulika na tatizo hilo ndivyo itakavoamua matokeo yake kiafya aidha mazuri au mabovu. Msongo wa mawazo huisha pale tu kisababishi au hatari inapopita na kutoweka.
 
Moja ya njia hizo ni kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha na kupumzisha mwili, mwili unapokosa usingizi wa kutosha basi unapunguza uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo na hivyo kuongeza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo . njia zingine unazoweza kutumia ni hizi hapa
1. kushugulisha mwili mara kwa mara
2. kufanya mazoezi mepesi ya mwili
3. kubadilishana mawazo na watu wanaokuzunguka
4. tenga mda kufanya vitu vinavyokupa furaha
5. kusikiliza musiki na kufurahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…