Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Moja ya njia hizo ni kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha na kupumzisha mwili, mwili unapokosa usingizi wa kutosha basi unapunguza uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo na hivyo kuongeza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo . njia zingine unazoweza kutumia ni hizi hapa
1. kushugulisha mwili mara kwa mara
2. kufanya mazoezi mepesi ya mwili
3. kubadilishana mawazo na watu wanaokuzunguka
4. tenga mda kufanya vitu vinavyokupa furaha
5. kusikiliza musiki na kufurahi.
 
Njia mbaya za kuondoa msongo wa mawazo
Hebu tazama njia ambazo baadhi ya watu hutumia, njia ambazo hupunguza tatizo kwa muda mfupi na kulifanya tatizo kuwa kubwa zaidi baadaye:
· Kuvuta sigara
· Kunywa pombe sana
· Kula sana au kula kidogo
· Kukaa kwenye TV au kompyuta, saa nyingi sana
· Kujitenga na marafiki, familia na shughuli
· Kutumia vidonge
· Kulala sana
· Kuahirisha mambo
· Kujishughulisha saa zote kuepuka matatizo
· Kuwatulia wengine msongo wao (kubwatuka, kufoka, kupigana)
 
Kwa sababu kila mmoja wetu yupo tofauti na atakichukulia tofauti kinapotokea kitu cha kusababisha msongo wa mawazo, hakuna namna moja tunayoweza kusema ufanye linapotokea jambo fulani, hivyo basi itabidi ufanya utafiti na kuona ni njia zipi zinaleta mabadiliko kwako. Zingatia kile unachokimudu na utakochoona kuwa kinachokusaidia.
 
Kimsingi kuna njia kuu mbili; kubadili mazingira ya chanzo cha msongo ambapo unaweza kukikwepa au kukibadilisha na pili kubadilisha jinsi hatua unazochukua ambapo unaweza kubalika ili uendane nacho au kukabaliana nacho. Tutazielezea njia hizo za kuukabili msongo wa mawazo hapa chini:
 
Chunguza ratiba yako: Itazame kwa kina ratiba yako, majukumu yako na kazi ulizojipangia kwa siku. Kama mambo ni mengi mno, yagawanye kwenye makundi ya yale ambayo ni lazima yafanywe na yale ambayo ni muhimu kufanyika. Yale ambayo si ya lazima sana yaweke chini kabisa kwenye ratiba au yaondoe kabisa.
 
2. Badili Mazingira ya chanzo:
Kama inashindikana kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo, badilisha mazingira yake. Jaribu kufikiria ni nini cha kufanya ili chanzo hicho kisijitokeze tena hapo baadaye, hii inamaanisha kubadili namna yako ya mawasiliano au namna unavyoendesha shughuli zako.
 
Tumia muda wako vizuri: Kushindwa kutumia muda wako vizuri ni chanzo kikubwa cha kupata msongo wa mawazo. Unapokuwa umechelewa kukamilisha jambo lako, utalifanya bila utulivu na utakosa umakini. Lakini ukiwa na mpango mzuri wa muda wako, utafanya kila kitu mbele yako kiufanisi na bila kupatwa na msongo wa mawazo.
 
Badilika Kuendana Na Chanzo:
Kama huwezi kukibadili chanzo cha msongo wa mawazo, wewe badili mtazamo wako kuhusu chanzo hicho:
Kitazame chanzo kwa mazuri yake: Kitazame chanzo cha kero kwako kwa kutazama mazuri ambayo yanaweza kupatikana kutokana na chanzo hicho. Badala ya kulalamika na kukasirika kutokana na foleni ya magari, chukulia kuwa huo ndio muda mwafaka kwako kujipumzika au kusikiliza muziki unaaoupenda ndani ya gari yako.
 
Rekebisha viwango vyako: Moja ya sababu ya kujipa msongo wa mawazo ni kutaka kila kitu kiende sawa kwa kiwango cha hali ya juu. Usijiweke kwenye mtego wa kushindwa kwa kujiwekea viwango vya juu kiufanisi. Jiwekee viwango vinavyowezekana kwako na kwa wenzako na jifunze kukubali matokeo ambayo hayakufika kiwango lakini siyo mabaya.
 
Kubaliana Na Yale Ambayo Huwezi Kuyakabili:
Vyanzo vingine vya msongo wa mawazo huwezi kuvibadili wala kuvizuia. Huwezi kukizuia kifo cha mtu wa karibu yako, wala ugonjwa mkubwa, au mporomoko wa uchumi wa nchi. Hapa inafaa kukubaliana na hali ingawa ni vigumu, lakini ni bora kuchukua msimamo huo kuliko kugombana na kitu usichoweza kukibadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…