Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

'Kuvaa barakoa ninapowasalimia marais, mawaziri, maikteta, wafalme na malkia- kwa kweli sioni nikivaa.''

Lakini Trump amesisitiza mara kwa mara kuwa kuchagua kufuata muongozo wa wataalamu wa afya kuhusu barakoa ni suala la uamuzi binafsi.
 
MGONGANO BAINA YA HAJI MANARA NA ZAKARIA THABITI (ZAKAZAKAZI) .

"Nimemsikia Zaka Zakazi akisema ubingwa wetu wa kupewa, nawaheshimu sana Azam lakini wasisingizie tulibebwa, hii ni kukosa heshima watu tumeshinda back to back.
"Nimshukuru sana kocha wa Yanga Luc Eymael amekuwa mtu wa kwanza kumpigia simu kocha Sven kumpongeza kwa kutwaa ubingwa pia GSM amenipigia simu na kutupongeza pia "

"Sisi Azam ni wapinzani wetu ndani ya dakika 90' na si zaidi ya hapo. Tunawaheshimu Azam kama vile ambavyo tunawaheshimu Yanga .. lakini mtu kupata usemaji juzi basi anataka umaarufu.

[emoji3578]Haji Manara -Afisa Habari SimbaSc .

==={==============================

Zaka Zakazi Ameamua Kumjibu hivi ...

HOJA KWA HOJA

1. Kuhusu kuwaponda mabingwa.

Yawezekana ulihadithiwa na mtu ambaye hakuelewa nilichokisema, au ulisikia ukiwa kwenye mhemko mkubwa sana.

Sikuwaponda mabingwa na wala sikuwagusa popote, zaidi ya kuwapongeza. Niliwapongeza mapema, mara tu baada ya mchezo...tena kupitia vyombo vya habari na kupitia akaunti binafsi ya Instagram.

Lakini baada ya pongezi, nilitoa wito kwa waamuzi msimu ujao wafanye vizuri zaidi ya msimu huu ili bingwa asichafuliwe ubingwa wake kwa makosa yao.

Msimu huu ulikuwa moja ya misimu ambayo waamuzi wamefanya vibaya sana kiasi cha kamati ya waamuzi ya TFF kuvunjwa katikati ya msimu.

Kwa hiyo kusema waamuzi wajitahidi kupunguza makosa, ni kuwachafua mabingwa?

Au wewe hutaki waamuzi wakumbushwe kufanya vizuri?

2. Kuhusu kufungwa na Kagera

Hivi watu husahau walilotoka? Kwani nani hajawahi kufungwa na Kagera?

Aliyewapeleka Simba FIFA 2017, alikuwa nani?

Aliyesababisha makamu bingwa wa 2016/17 kususia tuzo za Vodacom ni nani?

Aliyesababisha kung'olewa viti uwanja wa taifa kwa mara ya kwanza kwenye historia ya uwanja huo mwaka 2013, alikuwa nani?

Aliyetoboa tundu 2018 pale uwanja wa taifa ni nani?

1997 aliyewanyima Simba ubingwa pale Kaitaba alikuwa nani?

Leo hii Azam FC kufungwa na Kagera ndiyo kipimo?

3. Kuhusu wafungaji

Kipimo cha ubingwa siyo lazima iwe mabao ya kinara wa orodha ya wafungaji bora.

Msimu wa 2011/12, Simba walikuwa mabingwa, na John Bocco wa Azam FC alikuwa na mabao 19.

Kinara wa mabao wa Simba alikuwa Emmanuel Okwi aliyefunga mabao 12.

Mabao mawili kati ya hayo, aliyafunga siku ya mwisho ya msimu, katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Yanga.

Mabao 5 kati ya hayo yalikuwa ya penati...kwa hiyo Simba hakustahili kuwa bingwa?

Ni kweli, mfungaji bora wa Azam FC hadi sasa ana mabao 8, lakini hajafunga hata moja la penati...na ligi bado haijaisha.
 
Kwako mwalimu kashasha
 
Katika kura ya maoni ya Ipsos ilibainika kuwa katika kipindi cha juma lililopita, 89% ya Wamarekani walivaa barakoa walipokuwa wanatoka nje ya nyumbazo-kukiwa na ongezeko la alama 20 kutoka katikati ya mwezi Aprili.
 
Trump amekua akikosolewa na Democrats kwa kupuuza kanuni ya uvaaji barakoa na kulifanya jambo hilo kuwa la kisiasa.

Lakini hivi karibuni vyombo vya habari vya Republican na Conservative vimeunga mkono suala la uvaaji barakoa.
 
Wakiwemo Makamu wa rais Mike Pence, anayeongoza kikosi kazi cha kupambana na Covid-19, Kiongozi wa wabunge wa seneti wa Republican Mitch McConnell, Seneta Mitt Romney na mbunge mwanamama Liz Cheney.
 
Siku ya Jumanne, seneta wa Republican wa jimbo la Tennessee Lamar Alexander alisema ni bahati mbaya kuwa ''hatua hii nyepesi ya kuokoa maisha imegeuzwa kuwa sehemu ya mjadala wa kisiasa ikisema ''kama unamuunga mkono Trump, hautavaa barakoa, ikiwa humuungi mkono utavaa.''
 
Siku hiyo hiyo, Mkurugenzi wa utafiti wa magonjwa Dkt Anthony Fauci aliwaambia wabunge kuwa inawezekana idadi ya watu wanaoambukizwa itafikia 100,000 kwa siku, na si Wamarekani wengi wanaovaa barakoa au kufuata kanuni ya kutochangamana.
 
Ongezeko la maambukizi limesababisha majimbo kadhaa kuahirisha mpango wa kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea.

Kanuni ya kuvaa barakoa katika maeneo ya Umma ni suala la lazima kwa majimbo karibu 20 nchini humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…