Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20200702-WA0009.jpg
 
*SIMBA SIMBA SIMBACERONA.......!!!!!!!*

*SULTAN WAWA:* Ukihitaji huduma yake kama kjn atakupatia kama Mzee atakupatia pia kaupiga mwingi xaana

[emoji871] *KENNEDY JUMA:* anaingia kwenye utaratibu mdogo mdogo tutaelewana tu.

[emoji871][emoji871] *SHOMARI SERGIO ROBERT SEMEDO ALEXANDER ARNOLD KAPOMBE:* Imeisha hiyo kazi kubwa assist bora [emoji17][emoji17][emoji17]Domayo ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga kwetu tunamwachia Mungu

[emoji871][emoji871] *MOHAMMED MARCELO ROBERTSON HUSSEIN ZIMBWE:* yaan yaan yaaan tosha ana kila ladha

[emoji871][emoji871] *MKUDE:* ni mkubwa kuliko ndemla anaanza yy anafata dogo good sana ile.

[emoji871][emoji871] *GERSON FRAGA VINHO DA SANTOS VIERA:* Nawaambia hivi viwanja vya kimataifa sio vibovu subiri shughuli yake. Sura nzuri roho mbaya ngoja nixeme tu huyu ni SERGIO BUSQUETS. Imeisha hiyo.

[emoji419][emoji419] *KACH FRANCIS BERNADO DA SILVA OZIL NYAMBURA KAHATA:* Ukitaka iliyochangamka anakupa ukitaka iliyo poa anakupa kifupi anakera kifupi ni fundi

*JOSEEE MESS LUIZ VINISIUS MIQUISSONE* hahaahaaa anakuita anakuchukua anakuhuriza mbio unaweza anafiti vizuri with a ball and without a ball

[emoji419][emoji419][emoji419] *CLATOUS INIESTA PIRLO CHOTA BRUNO HERNANDEZ CHAMA* [emoji23][emoji23][emoji23]nacheka kwa dharau halafu nachukua chupa ya maji nakunywa
Goli bora kwa mchezaji bora

[emoji419][emoji419][emoji419]JOHN JOHN YES PAPAA JOHN JOHN YES PAPAA JOHN JOHN YES PAPAA JOHN JOHN YES PAPAA
IMEISHA HIYO DE LA CAPTAIN

[emoji3][emoji3][emoji3]Jaman yule ndo Chama kama hajarogwa [emoji91][emoji91][emoji1491]

WANASEMAJE HUKOOOO
 
Baada ya Tangayika kuwa Jamhuri mwaka 1962 Adam Sapi Mkwawa alichaguliwa kuwa Spika wa kwanza wa bunge. Aliongoza hadi mwaka 1964 Tanganyika ilipoungana na Zanzibar na kuunda bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sapi akachaguliwa tena kuwa Spika na kuongoza hadi 1973, kabla ya Nyerere kumteua kuwa Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).
_
Akasimamia uchaguzi mkuu mwaka 1975, wakati Mwalimu Nyerere akishindana vikali na kivuli katika kiti cha urais. Yani ulikua unampigia kura Nyerere au kivuli. Hii ndio ilikua tafsiri ya demokrasia kwa Mwalimu Nyerere baada ya kufuta vyama vingi mwaka 1967. Funny [emoji1].!
_
Adam Sapi akamtangaza Nyerere kuwa mshindi wa kiti cha Urais kwa kupata 95% ya kura zote zilizopigwa na kivuli kupata 3.5% huku nyingine zikiharibika. Yani kuna 3.5% ya watanzania waliona heri kuongozwa na kivuli kuliko Nyerere. Interesting [emoji1787].!
_
Wakati Adam Sapi anaondolewa bungeni kwenda kuwa Mwenyekiti wa NEC, Erasto Mbwana Mang'enya alichaguliwa kuwa Spika wa bunge.

Baada ya Nyerere kukishinda kivuli chake mwaka 1975 na kupewa ridhaa ya kuongoza tena kwa awamu ya miaka mitano hadi mwaka 1980, alitamani Adam Sapi arudi bungeni awe Spika. Lakini Sapi hakuwa mbunge. Wakati huo sheria ya bunge no.3 inayoruhusu mtu asiye mbunge kuchaguliwa kuwa Spika ilikua haijatungwa.

Kwahiyo Nyerere alipeleka mapendekezo ya kubadili sheria ya bunge no.15 ili kumpa mamlaka Rais kuteua hadi watu 10 kuwa wabunge (wa taifa). Baadae marekebisho hayo ya sheria yaliwekwa kwenye Katiba ibara ya 67 kifungu (a) na (c).
_
Hapo Nyerere akapata uhalali wa kumteua Adam Sapi kuwa Mbunge na akachaguliwa tena kuwa Spika kwa mara ya nyingine. Akaongoza hadi mwaka 1994.

Na huo ndio ukawa mwanzo wa wabunge wa kuteuliwa na Rais (wabunge wa taifa). Marais wote waliofuata waliendelea kutumia kifungu hicho kuteua wabunge na wengine kuwapa uwaziri. James Mbatia, Prof.Sospeter Muhongo, Dr.Augustine Mahiga, na Dr.Philip Mpango, Dr.Tulia Ackson ni miongoni mwa watu walionufaika na fursa ya ubunge wa kuteuliwa na Rais.

Lakini hili ni wazo lililoasisiwa na Mwalimu Nyerere. Na kimsingi alimlenga "mshkaji wake" Adam Sapi lakini wazo hilo limeonekana ni la msingi na Marais wote waliofuatia wameliendeleza. Bila wazo hilo la Nyerere pengine tusingekuwa na akina Prof.Ndalichako, Prof.Kabudi, Dr.Mpango etc kwenye baraza la mawaziri.

Kwahiyo tunaona namna Nyerere alivyokua bingwa wa kubuni "theories" zake na kuzipretest. Zikubuma anazifutilia mbali na zikifanikiwa anazitungia sheria na kuzirasimisha. Zipo theories nyingi sana Nyerere amewahi kubuni wakati wa uongozi wake. Aliwahi kubuni kitu kilichoitwa mamlaka za miji na vijiji lakini zikabuma akazifutilia mbali. Alibuni pia mfumo wa elimu kwa wote kupitia "UPE" na mambo mengine mengi.

Marais waliofuata nao wamebuni "theories" zao lakini kwenye eneo la uongozi hakuna jipya. Wengi wamecopy na kupaste waliyoyakuta kwa watangulizi wao.

Kuuna makundi ambayo si majimbo lakini yalipaswa kuwa na uwakilishi bungeni. Kwa mfano "proffesional association" kama TLS, CWT, NBAA, etc kila moja itoe mbunge mmoja. Vyama vya walemavu kama viziwi, wasioona, walemavu wa viungo, walemavu wa ngozi kila kundi angalau mbunge mmoja. Online platforms nazo ziwe na uwakilishi angalau mmoja (blogs and social networks).
_
Tusiendelee kucopy na kupaste kila "theory" tunayoikuta ofisini. Tubuni nyingine pia. Nyerere angecopy na kupaste kila kitu kutoka serikali ya kikoloni leo tusingekua na wabunge wa taifa, na pengine hakuna Rais ambaye angekiria kubuni kitu kama hicho. Lakini Nyerere alibuni na wote waliofuatia wameiga. Waliopo madarakani sasa nao wabuni "theories" zao ili watakaofuatia waige.!
 
Back
Top Bottom