Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakikisha unapotumia simu yako haipati joto kali sana kwani mara nyingine hii inaweza kuwa na madhara ya moja kwa moja kama vile battery kulipuka au mambo mengine kama hayo. Pia mara nyingi simu hutoa kiasi kikubwa cha miozi au SAR pale simu inapokuwa inapata joto kali sana, hivyo simu inapokuwa na joto kali sana ni adui hata kwa afya yako mwenyewe hivyo akikisha una jitahidi kutumia simu ikiwa haipo chaji, pia chaji simu yako ikiwa iko kwenye sehemu yenye hewa na jitahidi kupunguza matumizi pale unapochaji simu yako.
 
Power Bank

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao mara nyingi wapo barabarani basi ni wazi unatumia Power Bank, kama unatumia vifaa hivyo basi ni vyema kuongeza uangalifu hasa pale unapoamua kununua power bank kwaajili ya simu yako. Mara nyingi power bank zisizo na ubora huwa na mtindo wa kuharibu batter ya simu yako kwa haraka sana hasa inapokuwa kwenye kifaa hicho kwa muda mrefu.
 
Hivyo basi jitahidi sana kununua power bank yenye uwezo mzuri ambayo itakuwa na uwezo wa kuchaji simu yako wa haraka na kwa muda mfupi ili kuepuka simu yako kuungana na power bank kwa muda mrefu. Jitahidi kununua power bank yenye uwezo wa 2A ambayo hii ni sawa na AC adapter.
 
Kuchaji Huku Unatumia Simu

asilimia kubwa ya watu wanachaji simu zao vibaya na hii kusababisha battery za simu kuharibika ndani ya muda mfupi sana. Baadhi ya battery za simu ni rahisi sana kuharibika kwa mtindo mbaya wa kuchaji hivyo ni muhimu kuwa makini.
 
Hakikisha usitumie simu yako huku unachaji kwani hii ni hatua ambayo inaharibu sana battery ya simu yako, kama una haraka sana ya kutumia simu yako washa flight mode pale unapokuwa unachaji simu yako itajaa chaji kwa haraka na utaweza kutumia ndani ya muda mfupi.
 
Kutumia Chaja Isiyo Sahihi

Imekuwa ni kawaida watu kuwaza kuwa chaji yoyote inaweza kuchaji smartphone bila kuwaza aina ya chaji inayotumia, mara nyingi watu hujali zaidi kuhusu simu zao kupata chaji kuliko kuangalia aina ya chaji inatumika kuchaji simu husika.
 
Mara nyingi kuna sababu za kampuni za simu kutengeneza chaja maalum kwaajili ya smartphone husika kwani teknolojia iliyotumika kutengeneza chaja hizo inakuwa inafanana au inaendana na smartphone husika, pia chaja hiyo inakuwa imepimwa na kuonekana kuwa na uwezo wa kutosha wa kuchaji simu husika.
 
Christopher Wallace alikuwa anasakwa na Polisi, Siku yupo nyumbani alipost picha kwenye Snapchat kuwa yupo hapo na Polisi kuona hilo walifika eneo hilo kwaajili ya kumkamata. Walimtafuta kila kona ya nyumba yake walimkosa mpaka Picha nyingine ya Snapchat ambayo alipost Christopher akitoa taarifa kuwa kajificha kwenye kabati, Polisi walipoenda kwenye Kabati hilo walimkuta jamaa katulia zake. Tukio lilitokea mwaka 2015.
Hahahaha
 
tanzania-flag.jpg
 
Back
Top Bottom