Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwanini kuna utofauti wa asilimia za gesi zinazounda ushuzi na harufu?Hii ni kwasababu hali ya ushuzi inatofautiana kwa mtu na mtu kutokana ni kiasi cha hewa aliyobugia, chakula alichokula na hali ya umeng’enyaji wa chakula tumboni.
 
Unaweza kushangaa ni kwanini unajamba lakini hakuna harufu mbaya inayotoka. Kiambata cha sulphur ndicho hufanya harufu kuwa mbaya zaidi ya kunuka, asilimia moja tu ya sulphur inaweza kuleta harufu mbaya kwenye ushuzi, kwahiyo kama aina ya chakula ulichokula kinategeneza sulphur kwa wingi basi ushuzi wako utakuwa unanuka.
 
Gesi iliyojikusanya tumboni hupita kwenye utumbo mdogo na baadae kutolewa nje kama unavyotoa haja kubwa. Wakati mwingine utoaji wa gesi hii unaweza kuambatana na maumivu hali inayoashiria pengine kuna chakula ulichokula kina tatizo, au hakijachakatwa vizuri na hivo kuchacha.Tatizo lingine kujaa gesi tumbo kiakwaida huambatana na kujamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…