Malisa GJ
Nimemsikiliza Uchebe akihojiwa na kituo kimoja cha radio anasema picha zilizopostiwa mtandaoni ni za mwaka jana na kwamba mwaka huu hajampiga Shilole kabisa. Anasema madai ya Shilole kupigwa siku ya sabasaba si ya kweli, kwa sababu hiyo siku Shilole hakulala nyumbani.
Ili kuthibitisha hilo amesema atafutwe akaguliwe kama ana jeraha lolote la hivi karibuni. Anadai Shilole ni mzima kabisa wa afya na hana jeraha. Uchebe anaeleza kuwa Shilole amekuwa na desturi ya kutokulala nyumbani hata siku mbili na akirudi hataki kuulizwa alikua wapi? Na hio ndio "source" ya ugomvi wao wa mara kwa mara.
#MyTake:
Kama asemayo Uchebe ni ya kweli, je yanahalalisha kosa la kumpiga mkewe kinyama kiasi kile? Je mke kutokulala nyumbani bila taarifa adhabu yake ni kipigo? Je kisheria jinai ina "expire" kama imefanyika muda mrefu uliopita? Kama ni kweli kipigo ni cha mwaka jana kwanini Shilole amepost leo? Na je alipopigwa alitoa taarifa polisi?