Kwa mfano, kama mko kazini na mlikuwa marafiki sana sana na mmoja akafukuzwa kazi na mawasiliano yakakoma ghafla tambua urafiki wenu uliunganishwa na hiyo kazi na huo haukuwa urafiki wa dhati bali wa kimasilahi au kikazi tu. Tambue hilo vyema ili lisikusumbue.
Au mlikuwa marafiki sana sana na unayedhani ni rafiki yako akapata kazi nzuri na urafiki wenu ukakoma ghafla tambua kwamba urafiki wenu ulijengwa katika kupiga story tu za vijiweni na haukuwa marafiki wa dhati kama ulivyodhani. Tambua hilo vyema ili lisikusumbue.
Tunakiwa kuwa na imani siku zote kwamba tuna nguvu za asili ambazo Mwenyezi Mungu ametupatia, tukiweza kugundua nguvu tulizo nazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na tukazitumia ipasavyo, hakuna wa kutuzuia katika kufanikisha kusudi la maisha yetu.
Kila siku unatakiwa kutambua kwamba; katika viumbe vyote Duniani ambavyo Mwenyezi Mungu aliamua kuviumba, binadamu Sisi tumepewa uwezo mkubwa, nguvu kubwa, maarifa mengi na ujuzi mwingi kuliko kiumbe yoyote yule.
Law and order exist for the purpose of establishing justice and when they fail in this purpose they become the dangerously structured dams that block the flow of social progress.” Martin Luther King, Jr
1. Saba Saba ni sikukuu inayoadhimishwa tarehe saba, mwezi wa saba (7 Julai) ambayo lengo lake lilibadilishwa kutokana na mabadiliko ya historia na siasa.