Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

19b908b3-a687-4ba1-abc4-169bdd359a39.jpg
 
Karibu aina zote za vyakula zaweza kutumika kutengeza supu. Ukianzia na vyakula vyenye asili ya wanyama (Mfano nyama na samaki), vyenye asili ya mimea Mfano matembele, bamia, mchicha, bilinganya na vinavyo fa nana na hivyo na vyakula vitokanavyo na mbegu za mimea mbalimbali mfano karanga, korosho, ufuta n.k.
 
Faida za supu ni nyingi, kwa ufupi ni kama ifuatavyo: Supu husaidia kuamsha hamu ya kula kwa yule aliyekuwa hana na humuongezea hamu ya kula kwa yule aliyenayo. Na hii hasa hupatikana iwapo supu itakuwa na viungo mbalimbali vyenye harufu na ladha tofauti.
 
Supu huficha ubaya wa ladha ya chakula iwapo itaandaliwa vizuri na kunywewa baada ya mlo. Iwapo itatokea mtu hakupendezwa na ladha au harufu ya chakula, supu humsaidia kuficha au kuisahau hadha hiyo. Hii humfanya aridhike kama vile tangu mwanzo amekula chakula kizuri (akipendacho). Kwa kuwa nivigumu kujua ni chakula kipi kitamfaa yupi, ni vyema kuwa na angalau supu pembeni kama ziada ya mlo.
 
Supu hurahisisha mlo kuwa kamili hasa kwa wale wasioweze kutafuna au kula vyakula vya kawaida, mathalani, wagonjwa, wazee, vibogoyo au watoto. Supu hutengenezwa kwa kuchanganya vyakula mbalimbali ambavyo kwayo kwa kawaida mtu hawezi kuvila. Mfano kwa mtu amwenye meno mazima atakula nyama, atakuwa sawa na mzee au kibogoyo atakae kunywa supu yenye mchuzi wa nyama usioungwa.
 
Supu huburudisha na kuchangamsha huku ikikupatia virutubisho kedekede kwa ajili ya afya yako. Badala ya kununua vinywaji baridi vyenye kuburudisha lakini visivyonufaisha mwili zaidi ya kukufilisi, ni bora kujenga tabia ya kujiandalia na kunywa supu.
 
Miongoni mwa faida za supu uwezo wake wa kupunguza kasi ya kuongezeka uzito wa mwili. Hii hutokea hasa kwa wale wanaotunza uzito wao usiongezeke, ambapo hupunguza kula na badala yake kunywa supu na kuifanya afya kundelea kuwa nzuri.
 
Vile vile supu hupunguza matumizi na upotevu wa mabaki ya vyakula. Mara nyingi mchuzi utumikao kutengeneza supu auhitaji vyakula kama vilivyo. Mathalani nyama au samaki vyaweza kuchunwa na mifupa yake huchemshwa kupata mchuzi. Au badala ya kutupa mifupa au majani basi unayatumia tena.
 
Back
Top Bottom