Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

utafiti Jeremy Meeks, Alikuwa anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za ujambazi mpaka kufikia hatua Polisi kuweka picha yake Facebook ili watu waweze kutoa ushirikiano kama watamuona. Kilichotokea, Picha yake ilianza kupata umaarufu kutokana na muonekano wake, Alipokamatwa na kwenda jela alianza kupata dili nyingi kutoka Makampuni ya Mitindo (Modeling) hata alipotoka alianza kufanya kazi hiyo mpaka sasa.
 
Kutokana na katazo la Serikali Marekani kwa makampuni mbalimbali kuacha kufanya kazi na Huawei' unaambiwa Tsh Trilioni 25 ya mapato ambayo yalikuwa yanapata makampuni kadhaa Marekani kutoka Kwa Huawei hawatapata tena sababu Huawei' wameanza kujiandalia vifaa vyao wenyewe ambavyo mwanzo walikuwa wakinunua kutoka Marekani.
 
Sokwe' huishi kiutawala kama Binadamu. Watawala mara nyingi huogopwa huwa wabinafsi na katili. Kutokana na hayo wengi huwa hawadumu sababu Hupinduliwa. Wanaokaa sana madarakani ni wale ambao hugawana na wenzake mali lakini pia ni hatari sababu kupinduliwa kunaweza kutokea muda wowote.
 
"Ni marufuku kuning'iniza picha zangu kwenye Ofisi zote za Umma, u-Rais si umaarufu ama kuwekwa ukutani, badala yake kila mmoja wenu aweke picha za watoto wake awe anazitazama kila anapofanya maamuzi ya nchi hii''- Volodymyr Oleksandrovych Zelensky, Rais mpya wa Ukraine.
 
Bugatti ya kawaida unapata kwa bei isiyozidi Bilioni 6.8. Kubadilisha Oili' pekee Tsh Milioni 57. Kubadilisha Matairi pekee Tsh Milioni 87. Kukodi kwa siku 1 tu ni Tsh milioni 45 Lakini sio kwaajili ya kufanyia starehe bali kwa kazi za kisanaa kama Filamu, video za muziki, kupigia picha n.k
 
Una uwezo wa kuudanganya ubongo wako kwamba umefanya jambo fulani japo hujafanya na ukajisikia vizuri. Mfano ukijihisi Umechoka sababu hukupata usingizi wa kutosha, una uwezo wa kuudanganya' ubongo kuwa ulipata usingizi wa kutosha na utajisikia vizuri kama ulipata kweli usingizi wa kutosha kumbe sivyo.
 
Back
Top Bottom