Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufaamiana na Uislamu. Taarifa za wakoloni Wajeruami mwanzoni wa karne ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.
 
Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufaamiana na Uislamu. Taarifa za wakoloni Wajeruami mwanzoni wa karne ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.
 
Wabena ni moja ya kabila ambalo lilijiwekea historia kubwa hasa pale kwenye vita kati ya Wakamba na Wazaramo kwenye miaka ya 1750. Mwanzoni kabisa kabila hili halikufahamika kama Wabena. Wabena walipata kuishi wakiwa na mahusiano mazuri na kabila la Wazaramo.
 
Historia ya Wabena inafafanuliwa kwa ufupi kuwa, kabla ya kabila hili kuwa katika ngazi ya kabila lilikuwa katika ngazi ya ukoo. Ukoo huo uliitwa Wang’hoo. Na ukoo huu ulipata kujulikana na Wazaramo na uli pendwa sana. Ukoo huu ulikuwa ukijihusisha sana na biashara zilizokuwa zikifanywa maeneo ya mwambao ambapo Washomvi walikuwa wenyejii.
 
Kulitokea wakati kuliingia watu kutoka katika ardhi ya Ukamba yaani Wakamba. Watu hao walivamia maeneo ya pwana na kufanya vurugu kwa Wazaramo na wenyeji wengine waliokuwa wakiishi kwenye maeneo hayo. Wakati huo Wakamba wakiingia kwenye ardhi ya Wazaramo, kulikuwa na Shujaa wa kizaramo aliyejulikana kwa jina la Bwana Pazi Kilama aliyekuwa akiishi maeneo ya Kinyangulu.
 
Kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikifanywa na Wakamba, baadhi ya wenyeji pamoja na Wafanyabiashara wa Kibena huko mwambao waliomba msaada kwa Shujaa pazi. Na kutokana na uwezo aliokuwa nao shujaa huyo, aliamua kwenda kuwapiga Wakamba. Lakini kabla ya kwenda kwenye vita hivyo na wakamba, Shujaa Pazi Kilama, alikusanya jeshi lake
 
Miongoni mwa wanajeshi walitoka kwenye ukoo wa Wang’hoo. Na kutokana na uhimara wao, walipigana kwa nguvu zote na kuwapiga Wakamba wote na kuwafukuza. Na mara baada ya vita kuisha, inasemekana kuwa Wang’hoo waliamua kuwa wakishinda vita watavunja silaha zao zote na kutafuta zingine kama tuu pakitokea vita nyingine.
 
Na alifanya hivi kwa lengo la kutunza kumbukumbu, kwani kila vita bwana Pazi alikuwa akiweka historia kwa lengo la Watu kuja kujifunza. Hivyo pazi aliamua kuwaita Wabena Migoha. Na kutokana na mahusiano mazuri Wabena walipata kuishi na kushirikiana na Wazaramo, walizaliana na kuongezeka na walitawanyika sehemu mbalimbali kutokana na shughuli zao.
 
Na mpaka Wazungu wanafika katika ardhi ya Tanzania kwenye miaka ya 1850, walikuta kabila linalojitosheleza na likiwa na watu wake wengi sana.. Na kutokana na mabadiliko ya waandishi wa kikoloni walijaribu kufupisha jina lile, yani kutoka Wabena Migoha na kuja kuwa Wabena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…