Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Wasukuma ina maana ya watu waupande wa kaskazini, lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano wasukuma hutumia alama ya utambulisho (dira) kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila, kwa mfano wa jina kama hili Kiya hili lina maana ya Mashariki ambako ni mawio ya jua, huu ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa kwa jina la kabila fulani, mfano mwingine ni upande wa Dakama ambapo yatambulisha kama eneo la unyamwezini lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa kusini