Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wasukuma ina maana ya watu waupande wa kaskazini, lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano wasukuma hutumia alama ya utambulisho (dira) kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila, kwa mfano wa jina kama hili Kiya hili lina maana ya Mashariki ambako ni mawio ya jua, huu ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa kwa jina la kabila fulani, mfano mwingine ni upande wa Dakama ambapo yatambulisha kama eneo la unyamwezini lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa kusini
 
upande mwingine ambao unapewa alama ya utambulisho ni UShashi maana yake ni upande wa kabila ya washashi na neno hili washashi ni mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa mara japo pia neno hili shahi linamaanisha kabila la wakurya ambalo pia mpanuko wake unakomea hapo,
 
ambapo zaidi ya hapo eneo zima la upande huo unamaanisha upande wa kaskazini na upande wa mwisho kutambulishwa ni Ngw’eli, neno hili halikupewa kabila na badala yake linawakilisha upande wa magharibi (dira), ambako ni machweo ya jua. " Wasukuma wenyewe hulirejea jina hili kama Basuguma kwa (wingi) na Nsuguma kwa (umoja).
 
Wasukuma huishi eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania karibu na mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria, na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya Nyamagana, mkoa wa Mwanza, upo pia kusini magharibi mwa mkoa wa Mara, w:Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Shinyanga. Eneo la kaskazini la makazi yao ni katika maarufu Plain w:Serengeti.
 
Familia za wasukuma wengi sana wamehamia maeneo ya kusini kuelekea maeneo ya mkoa wa Rukwa ambao baadae umegawanyw’a na kuzaa mkoa wa Katavi, wakipita maeneo ya kabila ya Wapimbwe. Na hivyo kufanya makazi katika eneo hili la kijiji cha Wapimbwe.
 
Eneo hili la wasukumaland ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita za mraba 910 hadi 1200 sawa na futi Kigezo:Kubadili:. Mwinuko wake unakadiriwa kuwa inchi Ishirini hadi arobaini (Kigezo:Convert/wa) ya ujazo wa mvua kutoka Novemba hadi mwezi Machi.
 
Kiwango cha juu cha joto hutegemea angalau ni kutoka Kigezo:Convert/ya wakati kiwango cha chini nyakati za usiku hushuka na kufikia 15 °C (59 °F). Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezeka kwa wakulima wa mbogamboga
 
Shughuli kuu za kiuchumi kwa wasukuma ni kilimo,uvuvi, ufugaji na biashara. Pamba ndio zao kuu la kibiashara kwa wasukuma, ambao pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku, mahindi,Viazi,Dengu na matunda(Kisiwani ukerewe) Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini mengineyo huchimbwa katika maeneo mbali mbali mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
 
Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali. Yafuatayo ni maeneo yaliyo na madini.

1.Mwadui (Huku kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa huipatia serikali pesa za kigeni) 2. Maganzo (Vilevile eneo hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui.)
 
Kihistoria kama inavyosimuliwa na wataalamu kama wakina Nkondokaya na wazee wa Tanga, wanasema kuwa mji wa Pangani ulianza kukua na kama unavyoonekana leo hii kuanzia miaka ya 1600/1700. Na mji huu ulipatwa kukuzwa na Wabantu ambao walikuwa wakifanya biashara na wageni kutoka mashariki ya mbali.
 
Na wakati mji huu unakuwa kulikuwa na maeneo ambayo yalipatwa kukaliwa na watu , maeneo hayo ni kama Hale, Maporomoko ya Muhembo na maeneo ya Mtindiro. Wanazidi kusisitiza kuwa mji huu wa Pangani wa sasa hivi ni mji wa sita kwani kabla ya hapo kulikuwa na miji mingine ambayo ilijengwa na kufa.
 
Ukweli ni kwamba habari za mji wa Pangani zinajitoikeza hata kwenye vile vitabu vya masimulizi ya wasafiri kutoka Ugiriki( Periplus of Erythrean Sea). Na tunapozungumzia habari za masimulizi haya tunapata kusoma habari za mji wa zamani wa “Rapta” uliopata kuwepo miaka ya 80(BK au BM)
Kwa upande wa machifu na viongozi mbalimbali waliopata kujenga historia ya mji wa Pangani, wanatajwa wakina Zume Seif, Zumbe Mwera,Zume Upanga na Wakina Zumbe Zuberi.
 
Asili ya jina hili Pangani linazua masimulizi mengi sana, hii inamaanisha kuwa kulizuka masimulizi mengi ambayo yalikuwa yanajaribu kusimulia asili ya jina Pangani. Kwa kumrejerea tena mwanahistoria Bwana Nkondokaya na masilimulizi niliyoyapata kutoka kwa watu wa Pangani, wanasema kuwa, asili ya jina Pangani linatokana na Pango au mapango yaliokuwa yakitumiwa na watu wa mwanzo kama makazi yao.
 
Aidha neno hili pangani ni la kibantu lenye maana ya pangoni kwani asilimia kubwa ya watu waliokuwa wakiishi kwenye mapango.
Haikuishi hapo bado wanasema kuwa asili ya neno Pangani linahusiana na biashara ya utumwa. Kwani mji wa Pangani ni moja ya mji wenye historia kubwa ya biashara ya utumwa. Wanasema kuwa neno Pangani linatokana na neni la kiswahili Pangani. Kwani watumwa walikuwa wakiletwa katika pwani ya Pangani, walikuwa wakipangwa kwa lengo la kusafirishwa kwenye majaazi. Na hivyo watu wakaamua kupaita Pangani kama jina la sehemu ambayo watu hupangwa kabla ya safari za majini
 
Kwa ujumla mji huu wa Pangani hasa kwa wakati huu ni moja ya sehemu za vivutio vya utalii nchini Tanzania. Kwani mji huu umehifadhi historia kubwa sana hapa nchini Tanzania tangu miaka ya 80 BK/BM mpaka leo hii. Wilaya ya Pangani ina majengo mengi ya kale na yanatumika kama sehemu ya utaliiLeo hii pangani ni moya ya wilaya inayopatikana katika mkoa wa Tanga na wakazi wake wa asili ni wazigua hasa wale Waluvu, kutoka kwenye kundi la Waseuta. Hii ndio habari na historia fupi ya mji huu wa Pangani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…