Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Peter alisema licha ya kuwapenda sana paka wote lakini Delilah alikuwa anampenda zaidi, na hata akiwa safarini alikuwa anapiga simu mara kwa mara ili kusikia tuu sauti ya paka wake huyo. Aliwahi toa wimbo pia kwaajili yake, unaitwa Delilah.
 
Mary alikuwa mpishi maarufu sana miaka ya 1900 katika mitaa ya New York US akiwapikia watu kwenye taasisi mbalimbali kama shule, hospitali nk, mwaka 1906 alipika chakula kilichowadhuru walaji 53 huku watatu wakipoteza maisha kwa Typhoid, toka hapo akabatizwa jina la Typhoid Mary.

Ubaya ni kwamba homa hii wakati huo ndio ilikuwa inaanza kuenea mjini humo, kwahivyo moja kwa moja ilitafsiriwa kwamba Mary ndiye msambazaji mkuu wa Typhoid kwa watu.

Kutokana na dhana hiyo serikali ya New York ilimtenga Mary na kumpeleka katika hospitali ya Riverside iliyopo mbali katika kisiwa cha North Brother. Mary hakuamini kama kweli serikali imemuona hafai na kumtenga eti kisa anaeneza typhoid.

"Daktari wangu ananiambia sina typhoid, wala sina hata dalili za typhoid, mimi ni mtu mzuri, iweje ninaendeshwa kama mtuhumiwa, kama mnyama?"

Mara kwa mara alipeleka mashtaka mahakamani kuishtaki bodi ya afya ya New York kwa kumtuhumu na kumtenga hadi mwaka 1910 alipoachiwa kwa makubaliano ya kwamba ataachana na kazi yake ya kupika baada ya kutengwa kwa miaka mingi.
 
Mary akatafuta kazi kiwandani, lakini huko malipo yalikuwa madogo, baadaye akaamua kubadiliaha jina na kujiita Marry Brown na akaaendelea kupika chakula kama kawaida, na sasa alikuwa mpishi katika hospitali ya wanawake ya Sloane New York.

Mwaka 1915 madaktari na manesi wa hospitali hiyo jumla yao 22 waliugua Typhoid, watatu walifariki, mpishi alikamatwa na kuwekwa Quarantine bila kujua ndio yule yule Mary Mallon aliyewekwa Quarantine mwanzo kwa miaka minne.

Alipogundulika kuwa ni yeye alitengwa akawa chini ya ulizi mkali kwa zaidi ya miaka 23 hadi anafariki November 11, 1938 akiwa na miaka 69. Ilikuwa hakuna hata kutoka nje hali iliyopeleka hata mwili wake kuparalyze.
 
Katika miezi hiyo 79 iliyothibitishwa na shirika la anga la Marekani NASA, Gulileo aligundua miezi minne iliyopewa jina la miezi ya Gulileo yaani Gulileo Moons ambayo ni Io, Ganymede, Europa na Callisto.Mbali na hilo pia Gulileo anatajwa kuwa ndiye mgunduzi wa saa ya mshale.
 
Katika miezi hiyo 79 iliyothibitishwa na shirika la anga la Marekani NASA, Gulileo aligundua miezi minne iliyopewa jina la miezi ya Gulileo yaani Gulileo Moons ambayo ni Io, Ganymede, Europa na Callisto.Mbali na hilo pia Gulileo anatajwa kuwa ndiye mgunduzi wa saa ya mshale.
 
Miaka 95 baada ya kufariki jino lake moja na vidole vyake vitatu kikiwemo kidole cha katikati cha mkono wa kulia viliondolewa na kuhifadhiwa katika makumbusho ya kihistoria ya Museo Galileo, Italia. Sababu ya kuondolewa ni kumbukumbu na upendo tuu.
 
Mwaka 1737 kundi la watu waliokuwa wanampenda Gulileo waliuvamia mwili wake mahala ulipokuwa umehifadhiwa na kuondoka na vidole vitatu pamoja na jino moja na kwenda kuvihifadhi katika chuo kikuu cha Padua alikokuwa anafundisha enzi za uhai wake.Hata hivyo baada ya viungo hivyo kukaa kwa miaka mingi, mwaka 1905 viliripotiwa kuwa vimeibiwa chuoni hapo.
 
Taarifa zaidi zilisema kuwa Paulo mwenyewe aliamua kuviuza ili ajipatie pesa, na hatimaye sasa vilikuwa vimepatikana baada ya ufuatiliaji mkubwa wa hati za mauziano, vilianza kuonyeshwa hadharani katika makumbusho hayo.
 
Anaitwa Desmond Thomas Doss aliyezaliwa Virginia US February 7, 1919 na kufariki March 23, 2006 akiwa na miaka 87. Huyu alikuwa mmoja wa wanajeshi wa US aliyeingia vitani na wenzake katika vita ya Okinawa Japan mwaka 1945 ambayo ilikuwa ni sehemu ya vita ya pili ya dunia.
 
Desmond aliingia vitani bila silaha kwasababu yeye alipewa kitengo cha utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanajeshi wenzake waliokuwa majeruhi, lakini mwisho wa vita alionekana ni shujaa aliyewaokoa wenzake 75 katika uwanja wa vita.
 
Back
Top Bottom