Manchester United walikuwa na hamu ya kumsajili beki wa Uholanzi Nathan Ake ,25, kabla ya kujiunga na Manchester City kutoka Bournemouth wiki hii.. (Sky Sports)
Beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng anasema kwamba hatosema hawezi kurudi katika ligi ya Premia. mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alihudumu msimu wa 2010-11 akiichezea klabu ya Manchester City. (Guardian)
Serikali ya Lebanon imesema kuwa mlipuko mkubwa ulioteteresha maeneo kadhaa ya mji wa Beirut umesababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate iliyokuwa kwenye bandari ya mji huo.
Watu wameonesha ghadhabu zao na kutoamini kuwa kiasi hicho kikubwa cha kemikali hatari iliwekwa kwenye ghala bila kuzingatia hatua zozote za usalama kwa zaidi ya miaka sita, kwenye eneo hilo ambalo liko karibu sana na eneo la katikati ya mji.
Serikali haijaeleza kemikali hiyo ilipotoka, lakini kiasi hicho hicho cha kemikali kiliwasili Beirut mwezi Novemba mwaka 2013 katika meli ya mizigo ya iliyokuwa na bendera ya Moldova, MV Rhosus.
Chombo hicho kinachomilikiwa na Urusi kilianza safari mwezi Septemba kutoka Batumi, Georgia kwenda Beira, Msumbiji.
Ilikuwa imebeba tani 2,750 za ammonium nitrate, ambayo huwa katika muundo wa madonge madogo madogo ambayo hutumika kutengeneza mbolea lakini pia inaweza kuchanganywa na mafuta kutengeneza vilipuzi kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini na katika sekta ya ujenzi.
Wakati ikisifiri kupitia mashariki mwa Mediterranea, MV Rhosus ilipata ''tatizo la kiufundi'' na ikalazimika kutia nanga bandari ya Beirut, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 iliyoandikwa na mwanasheria wa Lebanon aliyewawakilisha wafanyakazi wa meli hiyo.
Meli hiyo ilifanyiwa uchunguzi na maafisa wa bandari na ''kuzuiwa kufanya safari'', mawakili walisema. Sehemu kubwa ya wafanyakazi wake walirudishwa makwao, isipokuwa nahodha wa meli Mrusi, Boris Prokoshev, na wengine watatu walioripotiwa kuwa raia wa Ukraine.
Bwana Prokoshev aliliambia shirika la habari la Reuters siku ya Alhamisi kuwa meli hiyo ilikuwa inavuja, na kuwa ilipelekwa Beirut na mmiliki wake kwa ajiliya kubeba mzigo mwingine zaidi kwa sababu ya changamoto za kifedha.
Hatahivyo, wafanyakazi wa meli hiyo hawakuweza kubeba mzigo huo , na mmiliki aliposhindwa kulipa ada ya bandarini, mamlaka ya Lebanon iliizuia meli hiyo, alisema.