Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alianza mechi 14 katika mashindano yote msimu wa 2019-20 na amecheza mara mbili tangu kandanda kurudi nchini Uhispania mwezi Juni.
''Yalikuwa mazungumzo binafsi baina yetu. Aliamua kutocheza'', alisema Zidane. Yaliyosalia ni kati yangu na yeye lakini ni kwamba alisema asingependelea kucheza
City ilishinda 2-1 katika awamu ya kwanza nchini Uhispania mnamo mwezi Februari kabla ya mlipuko wa corona hatua iliyofanya mashindano hayo kusitishwa kwa takribani miezi mitano.
Bale ambaye alitarajiwa kuhamia katika ligi kuu nchini China na kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning msimu uliopita kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba amekuwa mtu tofauti katika wiki za hivi karibuni , ikiwemo kujifanya kwamba alikuwa amelala wakati Real Madrid ilipokuwa ikicheza mechi yake ya mwisho iliyowafanya kutawazwa kuwa mabingwa wa Uhispania.
Alipoulizwa iwapo hatma ya Bale ipo mikononi mwa Madrid , Zidane alisema: Sijui. Kwasasa ni mchezaji wa Real Madrid . Hilo halijabadilika. bado yeye ni mchezaji wetu, naheshimu hilo na namuheshimu yeye, kama mtu mwingine yeyote.''Aliamua kutocheza. Hicho ndio kitu ambacho naweza kusema.''
Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre -Emerick Aubemayang ,31, anakaribia kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo.. (Telegraph - subscription only)
Lazio wana imani ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Manchester City David Silva . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu.. (Sky Sports)
Klabu mpya ilioteuliwa katika ligi kuu ya Premia Leeds United wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina na Stuttgart Nicolas Gonzalez 22 utaogharimu £20m. (Mirror)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.