Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Je wajua wakati Meli maarufu ya kubeba abiria ya RMS Titanic ilipozama, wanamziki waliendelea kupiga mziki hatimaye kuzama pamoja na meli hiyo ? Mnamo mwaka 1912 trh 15 April, meli ya Titanic ilikita barafu (iceberg) karibia na fukwe za Newfound land na kusababisha meli hiyo kuzama. Wallace Henry Hartley amabaye alikuwa kiongizi wa bendi aliendelea kupiga mziki alipogundua meli inazama ili kuwatuliza watu walio na taharuki na kupambana kujiokoa. Inakadiriwa watu takriban 1,500 walizama huku watu takriban 750 walipona ajali hiyo. Watu waliofanikiwa kujiokoa walimshuhudia Wallace na bendi yake wakiendela kupiga mziki hadi kuzama na meli hiyo.Wallace pamoja na bendi yake wanakumbukwa mpaka leo kwa kitendo hicho cha ujasiri. Mda mchache baada ya Meli kuzama mwili wa Wallace ulitafutwa na ulikutwa na kifaa alichokuwa anapigia mziki (Violin). Inasemekana Wallace alizikwa na watu takriban Elfu moja huku watu Elfu 30-40 walisindikiza mazishi hayo huko Colne Uingereza na sanamu lilijengwa kwa ajili yake kama ukumbusho