Je wajua chuo cha kwanza Duniani kinatoka Africa ? Chuo cha University of Timbuktu ni chuo kilichotakana na mafundisho kwenye misikiti mitatu ndani ya mji wa Timbuktu ambako kwa Sasa ni nchi ya Mali ya Afrika magharibi. Katika karne ya 12 uchumi mji wa Timbuktu ulikuwa kwasababu ya biashara zilizokuwa zinafanyika. Bidhaa kama dhahabu, chumvi na viungo mbali mbali. Biashara hizo ziliufanya mji ukuwe na uwe sehemu ya kujifunza kwani ziliwavutiwa watu mbali mbali ikiwemo wasomi na hasa wanazuoni/wasomi wa kiislam. Msikiti wa kwanza wa Timbuktu ulijengwa kipindi mansa kankan mussa aliporudi kutoka safari yake ya kuhiji Mecca Katika ya watu 100,000 walioshi katika mji huo 25,000 walikuwa ni wanafunzi. Quran na mafundisho ya kiislam ndio yalikuwa yanafundishwa na kupewa kipaumbele zaidi lakini masomo mengine yalikuwa yanafundishwa kama, Medicine & surgery, anatomy, botany, evolution, physiology and zoology, astronomy, anthropology, cartography, geodesy, geology, mathematics, physics, chemistry, philosophy, language and linguistics, geography, history pamoja na arts