Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua kuwa kupandikiza kwa moyo (Heart Transplant) ndo huduma yenye gharama ya juu zaidi katika sekta ya afya? Gharama yake ni takribani $1,382,400 sawa na 3,187,123,200 Tshs. Gharama hiyo hutokana na upatikanaji wa kiuongo hicho muhimu cha mwili, Maandalizi ya mda mrefu ambayo yanasababisha foleni pamoja na uzito wa kazi inayoenda kufanyika na kumuuguza mgonjwa mda mrefu baada ya upasuaji ili afya yake iimarike. Huduma zingine zenye gharama ni kama Double Lung Transplant * $1,190,700 Intestine Transplant *$1,147,300 Allogenic Bone Marrow Transplant *$892,700 Single lung Transplant *$861,700 Liver Transplant *$812,500 Kidney Transplant *$414,800 Autologous Bone Marrow Transplant *$409,600 Pancreas Transplant *$347,000 Cornea Transplant *$30,200
 
Je wajua wajua ni uwanja gani wa michezo mkubwa zaidi duniani? Indianapolis Motor Speedway uliojengwa 12.08.1909 ni uwanja wa mashindano ya magari na pikikiki. Una ukubwa wa ekari 550 sawa na kilomita za mraba 2.3. Uwanja huu unasiti za watazamaji 400,000 huku za kudumu zikiwa 257,000. Uwanja huo ulitumia gharama za $3M (1909) kutengeneza amabyo ni sawa na $84,645,824.18 (2019) Mashindano maarafu yanayofanyika na yaliyowahi kuafanyika katika uwanja huo ni Indianapolis 500, Nascar Brickyard 400, Indiana 250, F1 US Grand Prix (2000 - 2007), Moto GP (2008 - 2015
 
Je wajua kuwa timu yenye mafanikio kuliko zote kwenye mchezo wa mpira wa miguu inatokea bara la Afrika? Team ya Al Ahly nchini Misri (Egypt), ambayo inajulikana Kama timu ya Karne katika bara la Africa imeshinda makombe (112) mengi zaidi kuliko vilabu vingine barani Afrika na Dunia Nzima. Uwezo wa klabu ya Alhaly umekuwa juu kulinganisha na timu nyingine barani Afrika na wanamichezo wanaifananisha na klabu za ulaya kutokana na mfumo wao wa uchezaji. Al Ahly pia wamefanikiwa kuweka rekodi ya ushindi katika baadhi ya makombe waliyoshinda. Pia wanashika nafasi ya pili kushinda makombe ya kimataifa duniani wakiwa na makombe (20) nyuma ya Real Madrid yenye makombe (26) National league titles 🏆41(Record) National Cup titles 🏆36 (Record) National super Cup titles 🏆11 (Record) CAF African Champions League 🏆8 (Record) CAF Super Cup Titles 🏆6 (Record) African cup winners Cup 🏆4 (Record) Arab Super Cup 🏆2 (Record) CAF confederations Cup 🏆1 Afro-Asian Club Championship 🏆1 Arab club Championship Cup 🏆1 Arab Cup Winners Cup 🏆1
 
Je wajua kuwa timu yenye mafanikio kuliko zote kwenye mchezo wa mpira wa miguu inatokea bara la Afrika? Team ya Al Ahly nchini Misri (Egypt), ambayo inajulikana Kama timu ya Karne katika bara la Africa imeshinda makombe (112) mengi zaidi kuliko vilabu vingine barani Afrika na Dunia Nzima. Uwezo wa klabu ya Alhaly umekuwa juu kulinganisha na timu nyingine barani Afrika na wanamichezo wanaifananisha na klabu za ulaya kutokana na mfumo wao wa uchezaji. Al Ahly pia wamefanikiwa kuweka rekodi ya ushindi katika baadhi ya makombe waliyoshinda. Pia wanashika nafasi ya pili kushinda makombe ya kimataifa duniani wakiwa na makombe (20) nyuma ya Real Madrid yenye makombe (26) National league titles 🏆41(Record) National Cup titles 🏆36 (Record) National super Cup titles 🏆11 (Record) CAF African Champions League 🏆8 (Record) CAF Super Cup Titles 🏆6 (Record) African cup winners Cup 🏆4 (Record) Arab Super Cup 🏆2 (Record) CAF confederations Cup 🏆1 Afro-Asian Club Championship 🏆1 Arab club Championship Cup 🏆1 Arab Cup Winners Cup 🏆1
 
Je wajua kuna binaadamu aliwahi kuogelea kilometer 225 baharini kwa mda wa masaa 50 na dakika 10 ? Veljko Rogošić raia wa Croatia ndo amayeshikilia rekodi ya kuogelea umbali mrefu bilaa kutumia viatu maalum vya kuogelea (flippers). Alianza kuingia kwenye tasnia ya michezo ya kuogelea mwaka 1959 na kushinda mataji mengi mpaka kupelekea kuwakilisha Taifa lake katika mashindano ya olympics.
 
Je wajua kuwa mchezaji Diego Maradonna alifunga goli la mkono almaarufu kama Hand of God ? Cha kustaajabisha au cha kufurahisha zaidi, katika mechi hiyo pia alifunga goli la karne. Diego Maradonna anajulikana kuwa miongoni mwa wachezaji bora waliwahi kutokea duniani na kwa karne ya 20, kama Ilovyo kwa Pele. Katika robo fainali za kombe la dunia iliyofanyika Mexico (1986)Timu ya taifa ya Argentina ilipangwa na Timu ya taifa ya Uingereza. Mechi hii ilikuwa na uhasama mkubwa kwani miaka minne kabla ya hapo (1982) nchi hizo zilipigana vita juu ya visiwa vilivyopo kusini mwa bahari ya Atlantic (Falklands War). Mechi hiyo iliisha 2-1 huku marodonna akipachika magoli mawili ya kihistoria. Baada ya kufunga goli la mkono aliwaambia wachezaji wenzake waeendelee kushangilia na kumkumbatia bila kujishuku ili muamuzi aruhusu goli. Baada ya mechi hiyo Maradonna alisema ushindi huo ni kama kisasi kwasababu watoto wengi waliuliwa kwenye vita hiyo.
 
Je wajua kuna binaadamu amewahi kupona baada ya milipuko ya bomu la nuclear mara 2 ? Hiroshima na Nagasaki ni miji miwili iliyopo nchini Japan inayojulikana dunia nzima baada ya kushambuliwa na mabom ya nuclear na nchi ya Marekani katika vita vya pili vya dunia. Wakati vita hiyo inaelekea ukingoni Japan ilikataa kusalimu amri kama ilivofanya Ujerumani 08/03/1945. Baada ya mashumbulizi hayo yaliotokea tarehe 6 na tarehe 9, Agosti 1945, watu zaidi ya 200,000 walipoteza maisha na wengine kupata madhara mengi ya kiafya amabayo athari zake zipo mpaka leo hii. Tsutomu Yamaguchi alikuwa mkazi wa Nagasaki Japan ambaye alienda mji wa Hiroshima kikazi kipindi ameajiriwa na Mitsubishi Heavy Industries na akiwa mjini Hiroshima bomu la nuclear lilipuka 06/08/1945 saa 8:15 asubuhi. Alirudi nyumbani kwake nagasaki siku moja baada ya tukio na alirudi kazini ndani ya siku mbili tarehe 09/08/1945 baada ya kuugulia maumivu. Asubuhi aliporejea kazini na kuanza kusimulia yalio mkuta,mlipuko wa pili ulitojea mjini Nagasaki. Serikali ya Japan inamtambua Yamaguchi kuwa mtu pekee aliye pona mashambulizi yote mawili ya mabomu ya nuclear. Yamaguchi alifariki dunia 2010 akiwa na miaka 93.
 
1597142666267.png
 
Da'Vinci

Je wajua kuwa kuwa aina ya Vifaru wanaotambulika kama Northen White Rhino wako hatarini kutoweka duniani ? Mwaka jana 2018 mwezi wa 3 Kifaru mwenye jina Sudan alifariki dunia Kenya akiwa ndo dume pekee aliyebakia duniani. Aliacha wengine wawili ambao ni majike na ndo Vifaru pekee wa aina hiyo waliobaki. Hii husabibshwa na ujangili kwani pembe za vifaru hawa zina thamani kubwa sana, mwaka 2017 zaidi ya vifaru 1000 waliuliwa sababu ya ujangili bara la Africa. Pia husmekeana kuwa pembe hizo hutumika kutengenezea dawa za ki asili japokuwa wanasayansi wanasema dawa hizo hazina msaada wa ki afya
 
Je wajua kuwa nguchiro anauwezo kuwinda, kumuua na kumla nyoka ? Kuna aina 34 ya mnyama huyu (nguchiro) anayepatikana mabara yote duniani kasoro Austarlia na Antartica. Nguchiro aina ya Indian gray Mongoose anawinda na kula nyoka hasa wenye sumu kali kama King Cobra amabaye sumu yake inaweza kumuua Binaadamu ndani ya dk 30. Anaepuka kudhurika na nyoka kwa kumkwepa kwa spidi na kumvizia apate nafasi ya kumngata kichwani na kumuua. Pia nguchiro anangozi yenye manyoya mengi yanayomzuia nyoka kuzamisha meno yake. Pia nguchiro anakitu kinaitwa acetylcholine receptors inayompa kinga dhidi ya sumu kali ya nyoka huyo.
 
Je wajua kuwa Marekani ndio Nchi yenye viwanja vingi vya ndege vingi zaidi ? Marekani ina viwanja 13,513 vya ndege ikifatiwa na Brazil yenye viwanja vya ndege 4,093. Marekani inaongoza kwa sababu ya ukubwa wa nchi pamoja na watalii wengi wanaoingia nchini humo kila siku. Marekani inapokea watalii Milioni 76.5 kwa mwaka. Pia watalii hutumia pesa nyingi sana katika nchi hiyo (Marekani) kuliko nchi zingine zote. Mwaka 2017 Marekani ilingiza $211B kupitia watalii wakifatiwa na ; Spain-$68B France-$61B Thailand-$57B United Kingdom-$51B Italy-$44B Australia-$42B Germany-$40B China-$36B Japan-$34B **Tanzania - $2B
 
Je wajua filamu ya kutisha "Paranormal Activity" iligharimu $15,000/34,506,000Tshs kutengeneza na kuzalisha faida ya $193M/443,977,207,636 Tshs? Filamu hii ilitengenezwa na mtu binafsi na kuzinduliwa kwenye tamasha la sinema mwaka 2007, ilinunuliwa na kampuni ya Paramount Pictures kwa $350,000 na kufanyiwa maboresho na kuachiwa mwaka 2009. Kitaifa (Marekani) ilizalisha $108M na $85M kimataifa.
 
Back
Top Bottom