Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua wakati Meli maarufu ya kubeba abiria ya RMS Titanic ilipozama, wanamziki waliendelea kupiga mziki hatimaye kuzama pamoja na meli hiyo ? Mnamo mwaka 1912 trh 15 April, meli ya Titanic ilikita barafu (iceberg) karibia na fukwe za Newfound land na kusababisha meli hiyo kuzama. Wallace Henry Hartley amabaye alikuwa kiongizi wa bendi aliendelea kupiga mziki alipogundua meli inazama ili kuwatuliza watu walio na taharuki na kupambana kujiokoa. Inakadiriwa watu takriban 1,500 walizama huku watu takriban 750 walipona ajali hiyo. Watu waliofanikiwa kujiokoa walimshuhudia Wallace na bendi yake wakiendela kupiga mziki hadi kuzama na meli hiyo.Wallace pamoja na bendi yake wanakumbukwa mpaka leo kwa kitendo hicho cha ujasiri. Mda mchache baada ya Meli kuzama mwili wa Wallace ulitafutwa na ulikutwa na kifaa alichokuwa anapigia mziki (Violin). Inasemekana Wallace alizikwa na watu takriban Elfu moja huku watu Elfu 30-40 walisindikiza mazishi hayo huko Colne Uingereza na sanamu lilijengwa kwa ajili yake kama ukumbusho
 
Je wajua takriban Popo milioni 10 hadi 15 husafiri kutoka Congo hadi Zambia kila mwaka? Watu wengi wanafahamu kuwa nyumbu ndo huwa wanasafiri kwa idadi kubwa kuzidi wanyama wengine. Nyumbu Milioni 1.5 husafiri kutoka Tanzania kwenda Kenya kila mwaka na kurudi ila kutafuta chakula chao kikubwa ambacho ni majani yenye virutubisho Bora zaidi. Aina ya Popo waitwao Giant fruit bats ambao husafiri kwanzia Mwezi October hadi December wakitokea Congo hadi hifadhi ya wanyama ya Kasanka National Park Nchini Zambia kutafuta aina ya Matunda yanayopatikana kipindi hicho ndani ya mwaka mzima. Hali hii inavutia Sana utalii kwa wingi katika hifadhi hiyo. Safari hizo zinatija kwenye ukuaji wa misitu sababu Popo hao wanasambasa mbegu kupitia kinyesi wakiwa katika hizo Safari zao.
 
Je wajua Farasi ndie mnyama anyeshikilia record ya kuuzwa bei ghali zaidi ? Farasi wa mashindano nchini Marekani aitwae Green Monkey aliuzwa kwa $16,000,000 sawa na Tshs 37,033,600,000. Uzuri wake na ubora wake kwenye mashindano ya Farasi ilipelekea kwa asilimia kubwa hadi Farasi huyo kuuzwa kwa Bei hiyo kubwa. Farasi huyo alikimbia umbali mita 201 Ndani ya sekunde 9.8 katika shindano lake la kwanza. alizaliwa mwaka 2006 na kuuzwa mwaka 2008 akiwa na miaka miwili. Farasi huyo alikufa mwaka 2018 mwezi wa 7.
 
Je wajua kuwa kuna binadamu anayeweza kuongea lugha 58? Ziad Youssef Fasah (65) raia wa Lebanon ambaye sasa anaishi Brazil anatambulika na Gunniess book of world records kuwa ndo mtu anayeweza kuongea lugha nyingi zaidi kuliko wote. Yeye mwenyewe anasema anaweza kuongea lugha 59, na yeye anaamini kuwa ni kipaji amepewa na mungu. Lugha ambazo Ziad anaweza kuongea ni Kama Albanian Amharic Arabic Armenian Azerbaijani Bengali Bulgarian Burmese Cantonese Cypriot (dialect of Greek) Czech Danish Dutch Dzongkha / Bhutanese English Fijian Finnish French German Greek Hebrew Hindi Hungarian Icelandic Indonesian Italian Japanese Korean Kyrgyz Laotian Malagasy Malay Maltese Mandarin Mongolian Nepali Norwegian Pashto Papiamento Persian Polish Portuguese Romanian Russian Samoan Serbo-Croatian Shanghainese (dialect of Wu Chinese) Singlish Sinhala Spanish Standard Tibetan Swahili Swedish Tajik Thai Turkish Urdu Uzbek Vietnamese
 
Je wajua kuna kipindi cha darasani kilidumu kwa masaa 54 ? Mwaka 2003 mwalimu Professor Marie Burrow katika shule moja huko laidlaw Queensland Australia.alifundisha wanafunzi 26 Somo la Biology kwa masaa 54 mfululizo sawa na siku mbili na ana shikilia rekodi hio mpaka sasa
 
Je wajua smart phone (simu janja) ya kwanza imetoka mwaka 1994 ? The IBM Simon ilianza kutengenezwa mwaka 1992 na kuingia sokoni mwaka 1994 Agosti na mauzo yalisitishwa 1995 Februari. Simu hii ilikuwa na uwezo wa touch screen pamoja na kutuma na kupokea email na fax, calenders, calculator na address book, notepad, 1GB RAM na flash storage, 16 megahertz processor Walifanikiwa kuuza units 50,000 za simu hii na wengi walikuwa wanapata changamoto jinsi ya kuitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…