Kukata tamaa kimekuwa kikwazo kikubwa cha kufikia mafanikio. Watu wanapokutana na mazingira ambayo siyo mazuri au rafiki kwao ,wanapokutana na matokeo kinyume cha matarajio huanza kuvunjika moyo na kushindwa kuendelea mbele.
Ipo faida kubwa kama utaendelea bila kugeuka nyuma na kuziangalia changamoto kama kizuizi cha mahali unapotaka kufika. Najua kufikia ndoto zako si jambo rahisi lakini ukiwa na moyo dhabiti utafikia tu.
Ipo faida kubwa kama utaendelea bila kugeuka nyuma na kuziangalia changamoto kama kizuizi cha mahali unapotaka kufika. Najua kufikia ndoto zako si jambo rahisi lakini ukiwa na moyo dhabiti utafikia tu.
Zifuatazo ni baadhi ya faida utakazopata kama leo hutakata tamaa:
Utakuwa umejifunza mengi
Kama hutakata tamaa ,utakuwa umejifunza mengi ambayo ni hazina yako na vizazi vyako. Utakuwa ni mwalimu wa watoto wako na wengine juu ya maisha kulingana na yale uliyopitia na hivyo kupitia shuhuda yako watoto wako na watu wengine watajifunza na kuwatia moyo kuwa kumbe kila kitu kinawezekana kama hatutakata tamaa.
Ndoto yako lazima itimie
Kama hutokata tamaa ni wazi kuwa mafanikio ni lazima kwa kuwa kila siku utaitumikia ndoto yako inayokupeleka kwenye mafanikio .Kila siku utakuwa ni mtu wa kufikiri na kutafuta mpenyo wa kufanikisha ndoto yako njema .Naam hutaacha kujaribu vingi na kutafuta ushauri kwa watu kujua namna gani utafanikisha ndoto yako .
Utapata fursa nyingi zaidi
Fursa humtafuta yule mwenye uwezo wa kukabiriana na changamoto nyingi za maisha .Watu wengi wamekosa kutumia fursa zinazowazunguka kwa sababu wanakata tamaa mapema sana. Ndiyo ukiendelea bila kukakata tamaa utakutana na fursa nyingi ,utakutana na watu sahihi na mambo mazuri mengi sana .
Utajenga heshima kwa watu na kukumbukwa
Watu wasio kata tamaa ni watu wanaoheshimiwa na jamii na daima wanakumbukwa sana hata wakitoweka duniani. Thomas Edson anakumbukwa kwa sababu hakukata tamaa, Jack Ma tumtaja sana kwa sababu hakukata tamaa.
Wakati mwingine inawezekana ukawa ni kinara mzuri wa kulalama juu ya maisha yako, huku ukisahau ya kwamba unachokizungumza mara kwa mara dicho ambacho kinasabaisha maisha hayo kuwa magumu zaidi.
Mara nyingine mdomo huumba hicho unachokizungumza, mara kadhaa nimekuwa nikiwasikia vijana kwa wazee wakisema vyuma vimekaza, hii ikiwa ina maana ya kwamba mambo ni magumu sana, wapo wengine ambao wanasema ya kwamba jamaa anabana, sijui ni jamaa gani?
Swali linakuja ni kwanini umeyaruhusu maisha yako yaongozwe na fikra za aina hii?
Nasema hivi nikiwa kifua mbele pasina kuona aibu, nikiwa na maana ya kwamba, watu wengi tupo vizuri sana katika kuzungumza matatizo yaliyopo kuliko kuzungumza suluhisho la matatizo hayo.
Yupo mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema katika maandiko yake ya kwamba, acha kuzungumza kuhusu matatizo bali zungumza kuhusu suluhisho la matatizo hayo, kwani kutumia muda mwingi kuzungumzia kuhusu matatizo ni kuongeza matatizo na si kupata majawabu.