Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1597315065503.jpg
 
Chama cha The Forum for Democratic Change (FDC) nchini Ugandakimejipata katika njia panda baada ya muasisi wa chama hicho na mgombea mara nne wa urais , Kizza Besigye, kukataa ombi la kupeperusha tena bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa ujao wa 2021.
 
Alikwenda mara mbili katika Mahakama ya juu mwaka 2001 na 2006 na katika kesi zote hizo kwa kauli moja majaji walithibitisha kuwa kulikua na wizi wa kura lakini kwa mgawanyiko wa kura mwaka 5:2 na 4:3 mwaka 2006 , huku wengi wa majaji wakiamua kuwa wizi wa kura haukutosha kubatilisha matokeo ya mwisho ya kura.
 
Uamuzi wa Dkt. Besigye wa kutogombea urais mwaka 2021 umekiacha chama cha FDC kikimtafuta atakayekiwakilisha katika uchaguzi huo.
 
Tayari chama hicho kimeaihirisha mara mbili uteuzi wa wagombea wake wa uraiskwa matumaini kuwa Dkt. Besigye angebadili msimamo wake na kuchukua fomu za uteuzi.
 
2019 mbunge wa upinzani Uganda Robert Kyagulanyi na mwanaharakati wa kisiasa na mpinzani Dkt Kizza Besigye waliahidi kushirikiana kukiondosha madarakani chama tawala National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.
 
Akizungumza na kituo cha televisheni cha NTV, Bwana Besigye alikataa kujibu swali juu ya iwapo atagombea urais 2021 au la. Mara nyingi alisisitiza kuwa swali hilo ni kosa. Alisema hakuna uchaguzi utakaomg'oa madarakani Rais Museveni
 
Hatuhitaji uchaguzi ili tupate uhuru. Mkakati unaopaswa kutuandaa kupigana kwa ajili ya nchi yetu uchaguzi awepo au bila uchaguzi," alisema Dkt Besigye ambaye ni mpiganaji wa zamani na daktari binafsi wa Museveni wakati wa vita vyao vya msituni vya kati ya mwaka 1981 hadi 1986 vilivyoweka madarakani vuguvugu la National Resistance Movement (NRM).
 
Safari ya kutaka kuwania kiti cha urais nchini Uganda ya Dkt Kizza Besigye haikuwa rahisi. Mara kwa mara alikatwa kufungwa na hata kupigwa na maafisa wa usalama hususan alipojaribu kutafuta haki juu yake ukweli kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais
 
Mwaka 2016 Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) tena na maafisa wa polisi.

Watu walioshuhudia kukamatwa kwake walisema alikamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.
 
Back
Top Bottom