Inawezekana ni stori nyingi umezisikia, kuona kwenye filamu au hata kuzisoma kuhusiana na meli kubwa kuwahi kutengenezwa, meli ya Titanic iliyozama mwaka 1912 ikiwa baharini kutoka UK kwenda Marekani, karibu tukujuze mengi zaidi kuhusu meli hii.
Meli ya Titanic iligharimu $7.5 million tuu hadi kukamilika kwake mwaka 1911, hii ni pesa ndogo kuzidi hata bajeti ya filamu zilizotengenezwa baadaye kuigiza tukio la kuzama kwake mwaka 1912. Filamu ya Titanic ya mwaka 1997 ilitumia zaidi ya $200 milions hadi kukamilika.
Zaidi ya wafanyakazi, wanaume 15,000 walihusika katika uundwaji wa meli hii huko Belfast, Ireland. Ilitumika miezi 26 kufanya kazi mpaka meli kukamilika, ni miaka miwili na miezi miwili.