Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1583098491558.jpg
 
Tani 22 za sabuni pamoja na mafuta vilimwagwa katika njia ambayo meli ilitakiwa kupita ili kuingia baharini baada kutoka kwenye sehemu ya matengenezo tayari kwa kuanza safari, zaidi ya farasi 20 pia walitumiwa kuivuta. Kulikuwa na urefu wa futi 772 hadi majini, ilitumia sekunde 62 tuu kuingia majini.
 
Ili mitambo yake kujiendesha meli ilikuwa inahitaji kuchoma karibu tani 600 za makaa ya mawe kwa siku moja yaliyokuwa yanatiwa ndani ya vifaa vyake na timu ya wanaume 176. Karibu tani 100 za majivu zilikuwa zinaingizwa baharini kila baada ya saa 24.
 
April 10, 1912 meli ilianza safari rasmi Southampton Uingereza kwenda New York US ikiwa na zaidi ya abiria 2,224 safari ambayo ilitumia masaa 28 tuu, mwendo wa kilomita 1,060 kabla ya meli hiyo kuanza kuzama baada ya kugonga jiwe kubwa la barafu. Hii ilikuwa ni safari yake ya kwanza.
 
Back
Top Bottom